In Summary

• Mzalishaji wa kazi nyingi za muziki wa Harmonize, Mr Simon alisema kwamba EP ya FOA haina mihemko kama ilivyotarajiwa na wengi.

Diamond Platnumz na Harmonize
Image: INSTAGRAM//

Mzalishaji wa kazi nyingi tu za msanii Harmonize, Simon kutokea nchi ya Norway amezungumzia kuhusu EP ya msanii Diamond Plaltnumz ya FOA ambayo imetoka wiki jana na kuwa gumzo kweli kweli kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na kituo kimoja cha habari nchini Tanzania, Mr Simon aliulizwa maoni yake ya kikweli kabisa kuhusu EP ya FOA na kusema kwamba ni hatua nzuri kwa msanii Diamond.

Alisema EP hiyo ni nzuri lakini kwake bado haijafikia viwango ambavyo alikuwa akivitarajia kutoka kwa msanii mwenye haiba ya kutukuka kama Diamond Platnumz.

Kulingana na produsa huyo, EP ya Diamond inakaa kawaida sana kama ngoma zingine tu na wala haina mabadiliko yoyote katika Sanaa ya Bongo Fleva.

“Ni EP nzuri na ni msanii mwenye kipaji, lakini kwangu mimi nahisi ni bado sana kulingana na chenye wengi walikuwa wanatarajia kutoka kwa msanii kama yeye. Ni ngoma nzuri na kubwa lakini si za kuchangamsha. Kwa sababu ni Diamond, tulitegemea vitu fulani vya kuchangamsha kwa sana, lakini sivyo kwai le EP. Lakini ni muziki mzuri,” alisema Simon.

Mzalishaji huyo wa muziki amefanyqa kazi na wasanii wengi utoka Tanzania lakini pia amefanya kazi nyingi mno na kwa ukaribu mkubwa na Harmonize ambaye kwa sasa ana timbwiri kubwa sana na Diamond Platnumz.

View Comments