In Summary

• Mchekeshaji Flaqo afikisha wafuasi milioni moja Facebook na kutoa video na muigizaji Carrol Sonia.

Mchekeshaji Flaqo na muigizaji Carrol Sonie
Image: YouTube screengrab

Mchekeshaji maarufu nchini Flaqo amefurahi kuwa miongoni mwa wakenya wachache wenye ufuasi wa watu zaidi ya milioni moja kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Mchekeshaji huyo anayefahamika na wengi kwa jina la uigizaji katika video zake fupi kama ‘Mama Othis’ amesherehekea hatua hiyo kwa kuachia wimbo mpya kwa jina la ‘Insincere’ ambao amemshirikisha aliyekuwa mpenzi wa mcheshi Mulamwah, Carrol Sonie kama video vixen.

Hii ni mara ya pili chini ya wiki mbili ambapo Sonie anaonekana kuzuga kama video vixen kwenye ngoma za wasanii wa humu nchini, ya kwanza ikiwa ni ile ‘Bingo Bango’ kutoka kwa msanii Madini Classic.

Wiki jana palizagaa uvumi mitandaoni kwamba Sonie huenda ameingia katika ulingo wa mapenzi na msanii Madini baada ya kuachana na Mulamwah, pindi walipoonekana katika picha ya pamoja ila ikaja kufahamika kwamba ni video ya ngoma walikuwa wanatayarisha.

Unahisi nini kinaendelea katika kichwa cha Mulamwah akiona aliyekuwa mpenziwe na mama wa mtoto wake aking’ang’aniwa na wasanii kuonekana katika video za ngoma zao?

View Comments