In Summary

•Ringtone amesema sababu kuu kwa nini hakushirikishwa kwenye shoo hiyo licha ya kuwa tajiri na maarufu ni kwa kuwa yeye ni msanii wa injili mwenye tabia nzuri.

Image: INSTAGRAM// RINGTONE APOKO

Mwimbaji wa nyimbo za injili Ringtone Apoko ameshtumu shoo maarufu ya 'Young, Famous and African' kwa kukuza tabia zisizowiana na maadili mazuri.

Msanii huyo aliyezingirwa na drama kochokocho katika taaluma yake amedai kwamba shoo hiyo ya Netflix ilishirikisha wasanii wasiokuwa na mienendo mizuri.

Ringtone amesema sababu kuu kwa nini hakushirikishwa kwenye shoo hiyo licha ya kuwa tajiri na maarufu ni kwa kuwa yeye ni msanii wa injili mwenye tabia nzuri.

"Sijaona mwimbaji wa injili pale. Labda wanatenekeza dhambi, walitaka wale watu wako na tabia mbaya lakini wamefaulu. Ukiangalia mimi niko na tabia nzuri na mimi ndiye mwenyekiti wa injili, hawataki watu wenye tabia nzuri," Apoko alisema akiwa kwenye mahojiano na Nicholas Kioko.

Ringtone hata hivyo alisisitiza kuwa amehitimu kushirikishwa kwenye shoo hiyo ambayo ilishirikisha wasanii maarufu na tajiri barani Afrika wakiwemo Diamond Platnumz, Zari Hassan na wengineo.

Alidai kwamba yeye ndiye mwanamuziki tajiri zaidi nchini Kenya huku akiwashtumu wasanii wenzake kwa kudanganya kuhusu utajiri wao.

View Comments