In Summary

• Fash Hussein, aliyekuwa mpenzi wa mchekeshaji DJ Shiti anadai alikula kiapo cha kutoikaribia ndoa hata kwa dawa

Aliyekuwa mpenzi wa DJ Shiti, Fazie Hussein
Image: Maktaba

Aliyekuwa mpenzi wa mchekeshaji DJ Shiti, Fash Hussein anahisi ni kama hatotaka kamwe kuolewa katika maisha yake.

Mama huyo wa mtoto mmoja alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na DJ Shiti lakini hapo kati boti likalemewa na mawimbi makali katika bahari ya mapenzi na kuzama ambapo penzi lao lilifikia kikomo.

Baada ya kimya cha muda wakiwa wametengana, Fash aliyaibua madai kwamba mchekeshaji huyo hakuwa anashughulikia mwanawe, madai ambayo Shiti aliyapuuzilia mbali na kusema kwamba yeye hushughulika kama baba.

Fash alizidisha kumwaga ubuyu zaidi kwa kusema kwamba kushughulikia mtoto kwenye Shiti alikuwa anadai ni kutoa shilingi 150 tu pesa za Kenya, na hili lilizua mvutano mkali baina ya wapenzi hao wa zamani mpaka kutupiana maneno ya akhera.

Wiki chache zilizopita, mwanamke huyo alitangaza kufikia uamuzi wa kumrudisha mtoto kwqa baba yake kutokana na kile alidokeza kama kufikwa na unyongovu na msongo wa mawazo.

Sasa anauliza wadau iwapo ni yeye tu amepigwa plasta na maisha ya ndoa mpaka anayaona mbinde au wako wengi.

“Ni mimi tu? Ama kuna wengine kama mimi ambao tumekula kiapo cha kutoolewa kamwe,” aliandika Fash kwenye instastories zake.

View Comments