In Summary

• Mwanahabari Willy Lusige ageuka gumzo baada ya kumsukuma mtu kwa kuingia mbele ya kamera.

Mwanahabari Willy Lusige akimfokea jamaa kwa kuingia mbele ya kamera.
Image: Screengrabs: Nairobi Gossip

Mwandishi wa habari kutoka kituo kimoja cha runinga nchini aliwaacha wengi katika hali ya mshangao mkubwa baada ya kumsukuma mtu aliyejaribu kuingia mbele ya kamera alipokuwa akiripoti mubashara kutoka nyanjani.

Willy Lusige alikuwa akiripoti moja kwa moja kutoka mkutano mmoja wa kisiasa kwenye kaunti ya Bungoma ambapo mtu mmoja aliyeonekana kujawa na furaha, pengine ya kupata nafasi ya kuonekana runingani katika nafasi muhali kama hiyo, alijaribu kudakia mbele ya mwandishi huyo wa habari, ila Lusige akamsukuma na kumfokea vikali.

Katika video hiyo fupi ambayo kwa sasa imesambazwa pakubwa mitandaoni, Lusige anaonekana akimfokea jamaa huyo ambaye hakupata nafasi ya kuonekana kwenye kamera japo hata kwa sekunde mbili.

“Baada ya kutembelea Busia katika mkutano wa Azimio la Umoja…” Lusige alikuwa ameanza kabla ya kitendo hicho kutokea.

Video hiyo sasa imepokelewa na watumizi wa mitandaoni na tayari wanaotengeneza jumbe fupi za kuchekesha, almaarufu ‘memes’ wameshazalisha jumbe zenye maudhui mbali mbali kutokana na video hiyo.

Wengine walifanya mzaha kwa kusema kwamba jamaa huyo alikuwa anataka kutuma salamu kwa watu wa kwao mubashara runingani lakini kwa bahati mbaya Lusige hakumpa nafasi hiyo ambayo jamaa alikuwa ameiona na kuikaribia kabisa.

View Comments