In Summary

• “Nafanya muziki Kama Hobby tu kwa hiyo sina muda wa kuhangaika kulipwa kutumbuiza" - Mobetto

Mwanamuziki Hamisa Mobetto
Image: Instagram

Mwanamuziki na mjasiriamali Hamisa Mobetto amewasuta mapromota wa muziki wanaowaita wanamuziki kutumbuiza na kisha baadae wakiambiwa gharama wanaruka juu ya kukataa kulipa kisa ni kubwa.

Amesema hiyo tu ndio sababu yeye aliamua kufanya muziki kwa ajili ya kujifurahisha tu na si kama kitega riziki kwani mapromota wanawatumia vibaya wasanii.

“Kwahiyo unaombaje msanii aje kufanya shoo, halafu baada ya kazi unadai ni ghali sana na kumfufua eti unaweza kupata msanii mwengine. Kwa nini usiende kwa wasanii hao wengine mwanzoni?” aliteta Hamisa Mobetto.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wake kuandaa matamasha makubwa ndani na nje ya nchi kama lile la Afro East Carnival la msanii Harmonize, Mobetto alisema kwamba yeye chaguo lake katika muziki ni kama ‘hobby’ tu kujibamba.

“Nafanya muziki Kama Hobby tu kwa hiyo sina muda wa kuhangaika kulipwa kutumbuiza kwa sababu najua tunaweza kunimudu, tutaishia kugombana,” alisema.

Hivi majuzi, msanii Ruby pia alilalamikia suala hilo la wasanii kutumiwa vibaya ambapo alilalama kwamba baadhi ya watu wanauliza bei yake kupiga shoo akishawaambia wanaanza kuteta kwamba ni ya juu na hata kumuapiza kwamba wasanii mbona wengi tu!

View Comments