In Summary

• Kampuni ya Netflix imesitisha mwendelezo wa filamu ya Fast and Loose yake muigizaji Will Smith bbada ya tukio la kumzaba kofi Chris Rock.

• Netflix walisema endapo filamu hiyo itaendelea basi itabidi Will Smith avulie kitengo alichokuwa akiigiza na kupewa mtu mwingine.

Muigizaji Will Smith
Image: Getty Images (BBC News)

Kampuni ya kusambaza filamu ya Netflix imempiga kifaa butu tena Kizito kichwani muigizaji Will Smith baada ya tukio la kumzaba kofi moto mchekeshaji Chris Rock katika hafla ya tuzo za Oscars wiki moja iliyopita.

Netflix ambao walionekana kuchukizwa na kitendo hicho kwa wiki moja sasa wameendelea kuachilia ghadhabu yao kwa Smith huku wakiendelea kumpogoa na kumparula kwa mwendo wa aste lakini wenye uchungu mno.

Baada ya kutangaza kujiondoa kuisambaza na kuionesha filamu ya Smith ya Bad Boys, sehemu ya nne, sasa pia imetangaza kusitisha kutoa huduma zake kwa filamu ya muigizaji huyo iliyotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni kwa jina Fast and Loose.

Katika maagizo mapya ambayo Netflix ilitoa kuhusu uwezekano wa filamu hiyo kuoneshwa na kusambazwa na kampuni hiyo, Netflix walisema kama itabidi kufanywa basi msanii Will Smith itabidi anyanganywe jukumu lake la ‘character’ ambaye alikuwa anaigiza na nafasi yake hiyo kukabidhiwa mtu mwingine tofauti.

Will Smith alishinda tuzo ya Oscars kama muigizaji bora katika tuzo hizo za Akademia zilizofanyika kwenye ukumbi wa Dolby jijini Los Angeles nchini Marekani mwishoni mwa mwezi machi.

View Comments