In Summary
  • Katika hafla hiyo Amber  alifichua kuwa anataka kuwaonyesha mashabiki wake sehemu nyingine yake
Amber Ray
Image: Elizabeth Ngigi

Mwanasosholaiti maarufu Faith Makau almaarufu Amber Ray amezindua rasmi taaluma yake ya Muziki.

Katika hafla hiyo Amber  alifichua kuwa anataka kuwaonyesha mashabiki wake sehemu nyingine yake.

"Kama Amber Ray, umenijua kama malkia wa maigizo, lakini nataka kutambulisha upande wangu mwingine ambao ni mfanyabiashara. Nina biashara nyingi sana... watu wamekuwa wakiniuliza nafanya kazi gani," Amber Ray alisema.

Mwanasosaolaiti huyo alifichua bali na kutoa vibao vipya atafungua studio yake ya kurekodi muziki.

"Leo nataka kutambulisha mojawapo ya biashara zangu ambayo ni lebo ya Rich Badness. Ambayo ni kampuni ya kurekodi...tunatoa maudhui ya tangazo kwa makampuni."

Siku ya Alhamisi alasiri, Amber Ray aliingia kama malkia katika maduka ya TRM, ambapo alifanya mkutano na waandishi wa habari.

Mwimbaji huyo mpya mjini alifichua kuwa hawezi kufukuza umaarufu ili kukuza muziki wake.

"Huwa sitafuti kiki...kiki huwa inanitafuta mimi," Alijibu Amber Ray.

View Comments