In Summary

•Harmonize amesema alichagua Range Rover kwa kuwa  anafahamu fika kwamba ndilo gari la ndoto za mpenzi huyo wake wa zamani.

•Gari alilonunua Harmonize limesajiliwa kwa nambari KAJALA 1 GP kuashiria kwamba alinunua maalum kwa mwigizaji ambaye alichumbiana naye kwa miezi michache tu.

Image: HISANI

Staa wa Bongo Harmonize bado hajakata tamaa katika kumbembeleza aliyekuwa mpenzi wake Fridah Kajala Masanja akubali ya kale yaishe na warudiane.

Siku chache tu baada yake kumnunulia Kajala mkufu wenye thamani ya Tsh5m, Harmonize amejitosa tena sokoni na kumnunulia mwigizaji huyo gari jipya aina ya Range Rover Evolve.

Harmonize amesema alichagua Range Rover kwa kuwa  anafahamu fika kwamba ndilo gari la ndoto za mpenzi huyo wake wa zamani.

"Natamani ujue kwamba nakupenda sana. Narudia tena, nisamehe na unipatie nafasi ya mwisho. Nakupenda, nirudie. Nakumbuka kuna siku ulishawahi kuniambia ni moja ya gari ya ndoto yako. Tafadhali jua nakupenda," Harmonize alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kupitia zawadi hiyo ya thamani, Konde Boy amemtaka Kajala afahamu kuwa anayajuta sana maovu aliyomtendea pamoja na familia yake hadi kupelekea kuvunjika kwa mahusiano yao.

Harmonize amemuomba Kajala msamaha na kumsihi warudiane huku akidai kuwa mama huyo wa mpenziwe Rayvanny ndiye mwanamke anayemfahamu na kumuelewa zaidi.

"Inaeleza Majuto Ya Yote Niliyo Kufanyia !!!! Ninacho omba Kwako ni Msamaha wa thati Ya Moyo Wako !!!! Frida wewe ni Mtu Wa Mungu Sanaa!!! Unasali Pia Bila shaka Unatambua Hakuna Mkamilifu Hutokuja Kuanza Upya Mama. Unanifahamu zaidi, rudi tena. Usisahau Mimi ni Mtoto wa Masikini Mwenzio Tu.  Nina Familia ,Wajomba, Shangazi Wadogo Na Ndugu Kibao Masikini Ambao Nikifa Leo Ndio Watakao Nizika Ila Nimeona Wewe Ndo Unastahili," Harmonize alimwandikia Kajala.

Gari alilonunua Harmonize limesajiliwa kwa nambari KAJALA 1 GP kuashiria kwamba alinunua maalum kwa mwigizaji ambaye alichumbiana naye kwa miezi michache tu.
View Comments