In Summary
  • Kulingana na Mtumba Man, Kinuthia ndiye alimpigia simu na kumwalika katika chakula cha mchana
Kinuthia na Mtumba Man
Image: Instagram//Kinuthia

Waunda maudhui Kinuthia na Mtumba Man kwa siku chache wamekuwa wakivuma sana mitandaoni baada ya madai wawili hao wanachumbiana.

Mtumba Man akiwa kwenye mahojiano alikana madai hayo na kusema kwamba hawana uhusiano wa kimapenzi na Kinuthia ilhali walikuwa wanaunda maudhui.

Kulingana na Mtumba Man, Kinuthia ndiye alimpigia simu na kumwalika katika chakula cha mchana.

"Sioni shida na Kinuthia ako sawa ni mimi nitamuua mtu wa kuchumbiana naye wakenya hawawezi niamulia kwa sababu maisha ni yangu, siwezi ambiwa nimchukue Akothee, Avril lakini siwapendi

Aliponialika katika chakula cha mchana tulifanya mambo mengi kwa sababu sisi ni waunda maudhui na tunataka kujiunga na muziki, hatujafanya kitu chochote na Kinuthia cha Kimapenzi

Pia muunda maudhui huyo alisema kwamba mama yake akimkuballishia kumchumbia Kinuthia atakubali.

"Mama yangu akiniambia nimchumbie Kinuthia nitakubali," Alizungumza Mtumba Man. 

View Comments