In Summary

•Odemba ameweka wazi kuwa Ibraah ndiye mume wa chaguo lake huku akitangaza kuridhika na mahaba yake.

•Amesema kuwa amevutiwa sana na sura ya Ibraah, mchezo wake wa kitandani na maisha yake rahisi yasiyozingirwa na drama.

Image: INSTAGRAM// IBRAAH

Mwanamitindo Miriam Odemba amethibitisha kuwa yupo kwenye mahusiano na mwanamuziki  Ibrahim Nampunga almaarufu Ibraah.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram, Odemba ameweka wazi kuwa Ibraah ndiye mume wa chaguo lake huku akitangaza kuridhika na mahaba yake.

Malkia huyo mwenye umri wa miaka 40 ameeleza kuwa tayari amezama kabisa kwenye mahaba ya Ibraah.

"Nimemkolea Ibraah kwa sababu mtoto laini, mtoto safi, mwanaume asiye na maskendo na ndiye mume wangu mupige mniue. Huku chuma, huku sumaku niwaibie siri kabisa kwa hili Miriam Odemba siambiliki kabisa kwisha yenu habari," Odemba amesema.

Ameendelea kueleza sababu zake kutoka kimapenzi na msanii huyo wa Kondegang licha ya pengo kubwa kati ya umri wao.

Odemba amesema kuwa amevutiwa sana na sura ya Ibraah, mchezo wake wa kitandani na maisha yake rahisi yasiyozingirwa na drama nyingi.

"Hana maskendo ndioa maana napenda kukufa huyu mwanaume. Hilo swala la kuhangaika na watu wazima wenzangu kama wengine wanavyosema kwa sasa kwangu lipo likizo na inatakiwa mjue kwamba ukubwa jalala mtu mzima ni kutafutiana lawama za kutoridhishana mahabani. Sasa  ya nini yote hayo mimi sitaki lawama!" Odemba amesema.

Mwanamitindo huyo ameambatanisha ujumbe huo wake na picha ya Ibraah akiwa hajavalia  shati.

Siku za hivi majuzi kumekuwa na uvumi mwingi kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano baada yao kuonekana pamoja mara kwa mara na kusifiana hadharani.

Odemba amempiku Ibraah kiumri kwa takriban miaka 17.

View Comments