In Summary
  • Mwanasosholaiti Amber Ray amekuwa akivuma kwa muda kwenye mitandao ya kijamiim kwa ajili ya maisha anayoishi
Amber Ray
Image: Hisani

Mwanasosholaiti Amber Ray amekuwa akivuma kwa muda kwenye mitandao ya kijamiim kwa ajili ya maisha anayoishi.

Siku ya Jumanne kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashauri wote ambao wanamchukia waweze kumpa block au kuacha kumfuata mitandaoni.

Pia aliwaambia kwamba wakati huu hawatamuweza.

"Masaa ni ya kununua pressure pills na painkillers,juu Weh 🤣🤣 hamtaniweza round hii…. Na Wasio nipenda Wakati wa kuni unfollow ndio huu pia… in fact, just block me!🤣🥳," Amber Aliandika.

Amber Ray anasema itabidi ampe bintiye masomo ya jinsi ya kupenda lakini muhimu zaidi ni wakati gani wa kuacha kupenda.

Mama wa mtoto mmoja anasema hakuwahi kufundishwa jinsi ya kuacha kupenda, lakini tu jinsi ya kupenda watu.

Amber anasema hataki binti yake apate uchungu ambao amekuwa nao kwa kupenda watu bila kikomo.

Nitamfundisha binti yangu jinsi ya kupenda, lakini muhimu zaidi jinsi ya kuacha. Sikufundishwa jinsi ya kuacha ..... Ilinibidi kujifunza mambo hayo kwa bidii. ! #amberthebrand," Amber Ray aliandika.

Mashabiki wa Amber Ray walitoa maoni yao kuhusu chapisho lake wakisema wanamsubiri mtoto wa kike.

Kwa wengine, hili lilikuwa dokezo kwamba anaweza kupata mtoto hivi karibuni.

Ingawa Amber anazungumza kuhusu kile atakachomfundisha binti yake, mapema mwaka jana alisisitiza kwamba hataki kupata mtoto mwingine.

 

 

View Comments