In Summary
  • Ndio katika kumlea mtoto kuna changamoto zake haswa kama wewe ni mama kwa wakati wa kwanza
Celestine "Selina" Gachuhi
Image: Hisani

Celestine Gachui alifahamika sana mitandaoni baada ya kuigiza katika kipindi cha Selina kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Maisha Magic East.

Mwigizaji huyo alibarikiwa na kifungua mimba wake wiki 3 zilizopita, ambaye kupitia kwenye chaneli yake ya Youtube amesimulia jinsi mwanawe amebadilisha maisha yake na jinsi amekabiliana na changamoto kama mama.

Ndio katika kumlea mtoto kuna changamoto zake haswa kama wewe ni mama kwa wakati wa kwanza.

"NIlikataa hospitali kwa siku chache,sikuwa najua kwamba mtoto alifaa kudungwa sindano, sikuelewa kwa nini lakini nilihisi kama moyo wangu ungetoka, baada ya kuruhusiwa na kuenda nyumbani nilishindwa nini nini kitatendeka, usiku singelala vyema," Alisimulia Selina.

Aliongeza;

"Nikiwa hospitali sikuwa naweza kutoa maziwa kwa hivyo nilikunywa dawa, baada ya kuenda nyumbani mtoto wangu alikataa kunyonya, sikuwwa nalala, nilikuwa naamka nikiwa nimeshtuka mtoto akilia,akipiga kelel nilikuwa naruka karibu nianguke

Nilikuwa nalala na taa kwa sababu nilikuwa na mshangao sana kwamba kitu kinaweza kutokea. Hospitalini, niliamka na hakuna taa mtoto alikuwa analia na nilishtuka sana. Nilitokwa na jasho kila mtoto alipokuwa akilia.”

 

 

 

View Comments