In Summary

•Zuchu alikiri kwamba hajawahi kuwa na uhusiano wa karibu na mjasiriamali huyo wa biashara ya nguo.

•Zuchu alidai akaunti yake ya Instagram ilikuwa imedukuliwa wakati Esma alikuwa unfollowed.

Image: INSTAGRAM// ESMA PLATNUMZ NA ZUCHU

Staa wa Bongo Zuhura Othman almaarufu Zuchu amepuuzilia mbali madai ya ugomvi kati yake na mfanyabiashara Esma Platnumz.

Msanii huyo kutoka Zanzibar ameweka wazi kuwa uhusiano kati yake na dada huyo wa bosi wake bado ni mzuri.

"Sina beef na Esma, sina ugomvi naye. Kila siku anasapoti nyimbo zangu na hata kwenye group ya ofisi anaandika kwamba mimi ni msanii anayemkubali. Pia yeye ni dada wa bosi wangu kwa hiyo siwezi kuwa na beef naye kabisa," Zuchu alisema katika mahojiano ya simu na mtangazaji wa Wasafi Media Ankali Mambi.

Binti huyo wa staa wa taarabu Khadija Kopa alithibitisha kuwa Esma hajawahi kumkosea kiasi cha kuzozana naye. 

Zuchu hata hivyo alikiri kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wa karibu na mjasiriamali huyo wa biashara ya nguo.

"Mara nyingi huwa tunakutana tu na kuzungumza hivo tu. Huwa tunakutana katika sehemu za umma au labda kwa bosi. Mara ya mwisho tulikutana hospitali na tuliongea maneno mengi pale. Hakuna beef," Alisema.

Zuchu alisema hajawahi kugombana na Esma na  kuweka wazi kwamba huwa wanasalimiana vizuri kila wanapokutana.

Alipoulizwa sababu zake za kum-unfollow mfanyibiashara huyo kwenye Instagram, Zuchu alieleza kuwa hilo lilitokea wakati  ambapo akaunti yake ilikuwa imedukuliwa.

"Waliunfollow watu wengi wakiwemo mamangu, kaka yangu. Ni hivo, inakuwa sijui nani amekuwa unfollowed. Asubuhi nilipoamka ndipo nikakuta habari zikivuma kuwa nimem-unfollow Esma," Alisema.

Mwanamuziki huyo alithibitisha kuwa yupo katika harakati za kuwafuatilia tena wote ambapo walikuwa unfollowed.

View Comments