In Summary

•Kulingana na Terence, si jambo la kushangaza wakati macelebs wanaomba mchango  wa pesa  wanapokumbana na matatizo

•Terence anadai kuwa wao pia  ni watu wa kawaida sawa na wengine.

Terence Creative
Image: Hisani

Mchekeshaji Terence Creative amejipata pabaya baada ya kauli yake  ya kuwatetea watu mashuhuri wa Kenya wanaoomba pesa baada ya kufilisika.

Baadhi ya watu mashuhuri wamekuwa wakiishia kutafuta usaidizi wa kifedha kutoka kwa mashabiki wao baada ya kukumbwa na  changamoto za kifedha.

Kulingana na Terence, si jambo la kushangaza wakati macelebs wanaomba mchango  wa pesa  wanapokumbana na matatizo

Anadai kuwa wao pia  ni watu wa kawaida sawa na wengine; na haipaswi kupuuziliwa kwa sababu  ya umaarufu wao.

Alitaja mifano mizuri ya wasanii ambao washaomba mchango wa pesa  ni pamoja na Akuku Danger  na Omosh- ambao walisaidiwa sana na Wakenya walipohitaji usaidizi.

Wacha niulize tu, mbona hampendi ‘celebrities’ tukiwaekea paybill number mtusaidie wakati tukona shida mnaona sisi ni binadamu kama nyinyi na pia tunashikangwa na shida kama nyinyi tu?”Terence Creative alihoji.

Akitoa maoni yake kutokana na hayo, Daddy Owen  alisema alidai kuwa kila mtu ako na shida zake.

Hatua ya watu mashuhuri kuonyesha maisha yao ya mazuri wenye mitandaoni inawafanya wanamitandao kuamini kuwa wana pesa za kutosha kuhudumia bili zao wakati wowote kuna shida.

”Shida ni “maceleb” waneweka picha za soft life  bro mtu akisota unaingia ground.. unapiga mboka unarudi  speaking from experience.. I know highs and lows of ths thing.. nilipiga low but sahii niko freshi barida..  its doable! But on a serious note, if the paybill is for a cause like helping the society or giving, I have seen Kenyans coming through.. so I guess many so called “celebrities” we should use our platforms in giving back, coz they participated as well in building who u r, remember the followers, the likes.. the shows.. the sales.. come from the collective society as a whole. Let’s give back.”  Daddy Owen alisema.

View Comments