In Summary

• Mama huyo alianguka ofisini na kuzirai kwa kupewa taarifa kwamba mwanawe hayuko kwenye orodha ya wahitimu.

Mwanamke aliyejawa na hisia za hasira na machungu
Image: The Star//Maktaba

Jarida moja nchini Ghana limeelezea jinsi mwanafunzi wa chuo kikuu alisababisha mzazi wake kuzirai kwa mshtuko wa moyo baada ya mzazi kugundua mtoto alikuwa mwaka wake wa pili katika chuo hali ya kuwa alikuwa amejiandaa kwa shughuli ya kuhudhuria sherehe za kuhafili.

Kulingana na jaridqa hilo, mzazi alikuwa muda wote anajua kijana yake alikuwa miongoni mwa mahafali wa mwaka huu na alipofika chuoni alijulishwa mtoto wake bado ako mwaka wa pili chuoni, mshtuko ukamkumba na kuzimia alipopewa taarifa hizo katika ofisi ya mkuu wa waanfunzi katika chuo cha sayansi na teknolojia cha Kwame Nkurumah.

Tukio hilo lilizua mjadaal mkali kwenye mitandao ya kijamii kwa maoni kinzani huku wengi wakiwataka wazazi kufuatilia masomo ya watoto wao haswa wale wa vyuo vikuu kwani watoto kama hao wengi wao ni watu wazima wenye umri wa miaka 18 kwenda juu na wanajiona ni wazima kujifanyia maamuzi pasi na kuwashirikisha wazazi.

Wanafunzi wengi wanapofika vyuo vikuu aghalabu hujisahau na kuingia makundi yasiyojali elimu na mwisho wa siku wanajipata kufeli katika mitihani na kulazimika kurudia huku nyumbani mzazi anajua mtoto anaendelea vizuri na masomo kwa dhana kwamba chuoni hakuna kurudia.

Wengine hulazimika kusitisha masomo yao kutokana na ukosefu wa koto, pengine walipewa na wazazi wao na wakaifyonza kwa starehe badala ya kulipia mitihani.

View Comments