In Summary

•Ian aliweka wazi kuwa alizaliwa katika familia ya kikristo lakini akabadilisha dini na kuwa Buddha baadaye maishani.

•Alifichua kuwa alisoma kuhusu Ubudha kwa mara ya kwanza katika kitabu alicholetewa na rafiki yake.

•Hapo awali mamake alikuwa akipinga hatua yake ya kubadili dini  na kudai alikuwa akidanganywa.

Image: INSTAGRAM// IAN NENE

Muigizaji wa zamani wa kipindi cha Machachari, Ian Nene almaarufu Almasi, amezungumza kuhusu safari yake ya kubadilisha dini kutoka Ukristo hadi Ubudha.

Katika mazungumzo na Shivani Pau kwenye YouTube, Ian aliweka wazi kuwa alizaliwa katika familia ya kikristo lakini akabadilisha dini na kuwa Buddha baadaye maishani.

"Nilipokuwa mdogo tulikuwa na mambo ya kiroho katika nyumba yetu. Nilizaliwa na kukulia katika nyumba ya Wakatoliki. Mambo ya kiroho na dhana ya Mungu vilikuwepo kila wakati lakini si kama jinsi ambavyo ningetaka iwe. Kulikuwa na maswali ambayo ningeuliza na singepata majibu ya wazi," Ian alisema.

Alifichua kuwa safari yake ya kubadilisha dini iling'oa wakati akiendeleza masomo yake katika chuo kikuu nchini Uingereza.

Ian alifanya Digrii ya Uuzaji (Marketing) katika Chuo Kikuu cha Kent kilicho London na kuhitimu mwak wa 2019.

"Siku zote nilikuwa mtafutaji na siku zote nilitaka majibu. Siku zote nilikuwa nikidadisi kama vile lazima kuwe na kitu cha juu kuliko sisi wenyewe,"  Alisema.

Muigizaji huyo alifichua kuwa alisoma kuhusu Ubudha kwa mara ya kwanza katika kitabu alicholetewa na rafiki yake.

Wote wawili walikuwa wakivuta bangi na kushiriki mazungumzo wakati  rafikiye alipomkabidhi kitabu hicho alichopewa na mtawa.

"Niliangalia nyuma ya kitabu hicho nikaona sura ya mmoja wa waanzilishi wetu. Hata nilikuwa naweka jivu kwa uso wake. Nilikuwa nakiangalia na kusema, 'tunaweza kutumia karatasi zake kufungia bangi.' Kwa namna fulani nilikiweka, nikapanga na vitu vyangu na kuenda nyumbani kwa familia yangu," Alisema.

Ian alisema aliporejea nchini Kenya alipokea habari za kusikitisha zilizobadili mtazamo wake wa maisha.

Mama yake alimpa taarifa kuwa aligundulika kuwa na saratani ya matiti, habari ambazo zilimfanya apatwe na msongo wa mawazo.

"Nilikaa katika chumba changu na kuhoji Mungu, "ikiwa kweli upo, mbona unaruhusu mambo mabaya kuwatendekea watu wazuri?" Mama yangu hakuwa anahudumia familia yetu tu ila hata watu wengine katika jamii.. nilimuomba Mungu anifafanulie kwa kuwa mwenyewe sikuelewa," Alisema.

Ian alipokuwa akitafakari aliona picha ya mwanamke mfuasi wa madhebehu ya Zen na kutaka kujua zaidi.

Baadae alianza kuenda hekaluni na kujifunza mengi kuhusu dini ya Budhaa. Pia alianza kusoma vitabu kuhusu dini hiyo.

Muigizaji huyo alifichua hapo awali mamake alikuwa akipinga hatua yake ya kubadili dini  na kudai alikuwa akidanganywa.

View Comments