In Summary

• "Tumepokea malalamiko kuhusu akaunti yako kufuatia matamshi ya ‘Malkia Elizabeth hakuwa anapendwa kikamilifu katika bara la Afrika’” sehemu ya notisi ilisoma.

Mwanahabari Larry Madowo achukizwa na kitendo cha Twitter kumpa notisi
Image: Twitter

Mtangazaji wa runinga maarufu nchini na Kimataifa Larry Madowo amegadhabishwa na kitendo cha kampuni ya mtandao wacTwitter kumtumia notisi ya kuchunguza ujumbe wake aliouandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema kwamba malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili hakuwa anapendwa na kila mtu kote duniani.

Madowo alipakia picha ya notisi hiyo aliyotumiwa na mamlaka ya Twitter kwa njia ya barua pepe.

Hii ni baada ya ripota hiyo wa CNN kuandika na kusoma ripoti kwamba baada ya kifo cha malkia Elizabeth wa pili kuwekwa wazi wa ikulu ya kifalme Uingereza, baadhi ya Wafrika haswa nchini Kenya walisema hawahuzunishwi na kifo chake kwa kile walisema kwamba ukoloni wa Uingereza uliwatesa mababu zao enzi wakipigania uhuru wao barani Afrika.

Katika video aliyoisoma moja kwa moja kweney runinga ya CNN, Madowo alisema kwamba baadhi ya ripoti alizokusanya kutoka kwa watu walidinda vikali kumuomboleza malkia huyo kwani kifo chake kinawakumbusha madhira babu zao walipitia mikononi mwa wakoloni hao.

Madowo alisoma ripoti ya kiongozi wa upinzani wa South Africa Julius Malema na chama chake chake uliosema kwamba:

“Hatumuombolezi Malkia Elizabeth kwa sababu kwetu kifo chake ni kumbulo la wakati mgumu sana katika taifa letu na bara la Afrika,”

Mwanahabari huyo baadae baada ya kuandika kwenye Twitter yake kuhusu suala hilo, alipokea notisi kutoka kwa wakuu wa Twitter uliomwambia kwamab umeanzisha uchunguzi dhidi ya maneno yake kwamba Malkia Elizabeth hakuwa anapendwa kote katika bara la Afrika.

“Twitter inahitajika na sheria ya Ujerumani kutoa notisi kwa watumizi wake wanaoripotiwa kutoka Ujerumani kupitia sheria ya mtandao. Tumepokea malalamiko kuhusu akaunti yako kufuatia matamshi ya ‘Malkia Elizabeth hakuwa anapendwa kikamilifu katika bara la Afrika’” sehemu ya ripoti hiyo ilisoma.

Aidha baada ya mamlaka hiyo kudadisi kwa muda, walimuambia Madowo kwamba walipata maneno yake hayo hayakuwa na ubaya wowote na hawawezi kuyaondoa kweney Twitter.

“Tumechunguza matamshi yako yaliyoripotiwa na tumepata kwamba hayana madhara ya kusababisha yaondolewe kulingana na sheria za Twitter,” walimueleza.

Akionesha kughadhabishwa kwake na uchunguzi huo dhidi ya ripoti yake, Madowo alisema kwamab watu wengine hawapendi wakati Waafrika wanazungumza ukweli wa historia zao.

“Baadhi ya watu hawapendi Waafrika wanaposimulia hadithi zao (zake),” Madowo alisema kwa hasira.

 

View Comments