In Summary

• Shabiki wake mmoja alimwambia aanze na kumrekebisha mkewe ambaye kulingana na shabiki huyo anaweka mtindo wa dredi kichwani.

Muthee Kiengei awataka wanadada kujifunza kutoka mtindo wa nywele wa margret na rachael ruto
Image: Facebook//Muthee Kiengei

Mchekeshaji na mchungaji Muthee Kingei ameonekana kufurahishwa na jinsi mama wa taifa anayeondoka Margret Kenyatta na yule anayeingia Rachael Ruto wanavyojinadhisha haswa katika vichwa vyao.

Kiengei kupitia ukurasa wake wa Facebook, alipakia picha ya pamoja ya wawili hao wakiwa wanatembea kwa pamoja huku wakiwa wamejawa na tabasamu.

Mama Margret Kenyatta na mama Rachael Ruto wamejulikana kwa kunadhifisha vichwa vyao kwa nywele fupi pasi na vipodozi vyovyote kama mawigi na nywele za kubandika, mtindo ambao umekumbatiwa sana na wanawake wengi amabo wana dhana kwamba kuonekana wa kisasa lazima uwe ya mindo wa kusuka nywele wenye haiba ya kisasa.

Kiengei aliwapa changamoto wanawake kama hao na kuwataka kujifunza kutoka kwa maam hao wa taifa kwani licha ya cheo chao kikubwa katika uongozi wa taifa, bado wanajiweka katika mtindo wa nywele ulio wa kawaida kabisa.

“Kazi kwenu wanawake wale mnaangushwa na mawigi zingine mnakuna kuna na kalamu na kugonga gonga na ngumi kama mmefunga jicho moja ya kusikiza utamu wa mba.......Siri ndio hio hapa,” Muthee Kiengei aliandika huku akiwataka kuangalia picha hizo za Margret na Rachael.

Shabiki wake mmoja alimwambia aanze na kumrekebisha mkewe ambaye kulingana na shabiki huyo anaweka mtindo wa dredi kichwani na kumtaka Kiengei kuanza kutoka nyumbani kwamba.

Kwa utani, Kiengei alisema kwamba tayari ameshamnyoa kwa nguvu kwani kutoweka mtindo kama wa kina maam hao wa taifa ni kama kumzuia asiwe rais siku za mbeleni.

Nimemnyoa saa hii, anazuia nisikuwe rais kwa nini,” Kiengei alijibu.

View Comments