In Summary

•Sandra Mbuvi amewasuta wanamitandao wanaomfanyia matani na kumkejeli mwanasoshalaiti Vera Sidika kwa kufanya mabadiliko ya mwili yaliyomuacha na makalio madogo.

•Sandra aliwashauri wanamitandao kuacha kukejeli watu ambao hawajawakosea kwa jambo lolote kutokana na wasiwasi wao wenyewe.

Vera Sidika/Sandra Mbuvi
Image: INSTAGRAM

Bintiye Sonko, Sandra Mbuvi amewasuta wanamitandao wanaomfanyia matani na kumkejeli mwanasoshalaiti Vera Sidika kwa kufanya mabadiliko ya mwili yaliyomuacha na makalio madogo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sandra ameeleza kutoridhishwa kwake na kejeli nyingi ambazo mwanasoshalaiti huyo amepokea tangu alipofichua muonekano wake mpya siku ya Jumatano. 

Alihoji kwa nini wanamitandao walikuwa wakimhukumu mwanasoshalaiti huyo alipokuwa na makalio makubwa na pia  sasa wakati  ambapo amefanyiwa upasuaji wa marekebisho ya kurejesha makalio asili.

"Mbona mnachukulia kila jambo vibaya na kuona baya katika kila kitu? Inaudhi sana .Mlikuwa mnamhukumu Sidika alipokuwa na makalio makubwa kwa kuwa hakuwa na makalio asili na kuwa alikuwa amefanyiwa upasuaji ili kuyaongeza ila sasa ambapo ameamua kuwa na makalio asili na kufanyiwa upasuaji ili kutoa yale bandia mnamkejeli na kumshambulia kwa maneno mitandaoni," alisema.

Mfanyabiashara huyo ambaye alionekana kutopendezwa na maoni ya watu ambao walitafuta jambo lolote ili kumkejeli Sidika alibainisha kuwa hata  mke huyo wa Brown Mauzo awe na umbo lipi wanamitandao hawataridhika.

Sandra aliwashauri wanamitandao kuacha kukejeli watu ambao hawajawakosea kwa jambo lolote kutokana na wasiwasi wao wenyewe.

"Acheni kuonyesha wasiwasi wenu kwa watu wengine wasiowahusu na ambao watashinda na kufaulu mwishowe wa siku," mfanyibiashara huyo aliwafokea watu.

Hii ni baada ya Sidika kuanika picha yake mtandaoni iliyoonyesha upungufu wa makalio yake na kusema kuwa alifanyiwa upasuaji wa makalio ili kuyapunguza kutokana na sababu za kiafya.

Wanamitandao wamekuwa wakitoa hisia mseto baada ya mwasoshalaiti huyo kuonyesha mabadiliko makubwa ya mwili wake.

Vera Sidika/Sandra Mbuvi
Image: INSTAGRAM
View Comments