In Summary
  • Dakika chache zilizopita Eric Omondi alivunja ukimya kwenye mitandao ya kijamii kufuatia mmoja wa kipenzi na mshawishi wa mitndao nchini Vera Sidika
Image: Eric omondi Instagram

Dakika chache zilizopita Eric Omondi alivunja ukimya kwenye mitandao ya kijamii kufuatia mmoja wa kipenzi na mshawishi wa mitndao nchini Vera Sidika.

Eric Omondi ametoa matamshi yake kuhusiana na Vera Sidika ambaye amevuma mitandaoni baada  ya upasuaji wake kuathiri sekta ya burudani.

Kwa mujibu wa Eric Omondi, Vera Sidika ameteka hisia za Wakenya, jambo ambalo Watanzania na Wanigeria wamekuwa wakifanya.

Zaidi ya yote mchekeshaji huyo alidai kwamba wasanii wa kike nchini wamelala, na kwa hivyo wanahitaji kuamka.

"Sijali kile mnafikiria kuhusu Vera Sidika,kile najua chote amefanya tuongee,tumevutiwa na kupata umakini wetu wote PERIOD hivi ndivyo Watanzania na Wanigeria wamekuwa wakipata umakini wetu!!!

Na kisha akadondosha video ya Muziki ya HOOOOT🔥🔥🔥 bora kuliko 98% ya kile ambacho Wasanii wa Kenya Hutoa. Hiyo ni SHOWBIZ HAPO HAPO!!!

Alafu the fact that she had the Space to do it simply means watu Wamelala Fofofo, Hasa Wasanii wa Kike wa Kenya Uuuuuuuuuuuuuui😥😥😥😥😥🙉🙉🙉 @queenveebosset KUDOS👏👏👏👏👏👏."

Mapema wiki hii Vera aliwaacha wanamitandao na mazungumzo baada ya kufichua kwamba alifanyiwa upasuaji wa makalio.

View Comments