In Summary

• Mwanamume huyo alijiona kukosewa heshima na mwanadada ambaye alikuwa ameuenzi kiwango cha kumnunulia gari la kifahari.

Image: Facebook// Lindaikejiblog

Mwanamume mmoja nchini Nigeria alizua hali ya taharuki kwenye Klabu alipoharibu gari aina ya Range Rover ambalo alimnunulia mpenzi wake wa kando baada ya kudaiwa kumsaliti kimapenzi na mwanaume mwingine.

Mwanaume kutokana na hasira akaamua kuliharibu gari la kihafari aina Range Rover alilokuwa amemnunulia mpenzi wake.

Baada ya kitumbua kuingia mchanga na mwanadada huyo kufumaniwa, Mwanaume huyo alijiona alikuwa akisalitiwa na kukosewa heshima na mwanamume ambaye alitumia pesa nyingi kumzawidi na kumgharamikia mahitaji yake.

Mwanamume huyo alionekana kuzuiliwa na walinzi huku akimtemea laana anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa kando ambaye pia alijitolea hadi kufikia hali ya kumnunulia gari.

Huku akiyavunja madirisha ya gari mwanamume alisikika akimwita mwanadada huyo maneno yasiyoweza kutamkika hadharani au hata kuchapishwa.

Baadhi ya wapita njia walionekana kwenye video hiyo, wakimtaja mwanamke huyo kuwa 'mdanganyifa' huku wengine wakionekana kumlaumu mwanamume aliyeolewa kwa kukasirika.

''Angemnyanganya gari tu, Haina haja ya hasira''  Mwanamume mmoja alisema.

''Unamdanganya mkeo na unadhani wewe huwezi kudanganywa?'' Mwadada mmoja aliuliza.

Video kutoka kwa tukio hilo lilionyesha mwanadada huyo akijaribu kujinasua mikononi mwa jamaa ambaye alikuwa amejawa na hasira kama za mkizi.

Kulingana na vyanzo vya udaku, hasira za mwanaume huyo ziliongezeka hata zaidi baada ya kuaminika kupoteza takribani shilingi 54, 000 katika mchezo wa bahati nasibu.

View Comments