In Summary

"Amerudi? Hatimaye." Alisema jamaa mmoja.

Mwanamume mmoja aligeuka gumzo la siku baada ya kuwashtua watu aliposema kwamba alimwona ''Yesu''.

Mwanamume huyu alidai kuwa alimwona Yesu akiwa ameenda  nje kutembea na alipomwona kwa umbali aliamua kuchukua video ambayo baadaye ilipata watazamaji wengi.

Jamaa alisikika akisema, "ingawa siendi kanisani, huyo ni Yesu".

Kwenye Video hiyo, kwa mbali Yesu huyo alijongea huku akitembea kwa mkongojo na mwenye nywele ndefu jambo liliyofanya mwanamume huyo kuchanganyikiwa maradufu na kumwona kama ni Yesu Kiumbe anayedhaniwa kuishi milele.

Kwenye Video, Yesu huyo alitembea akiwa amevalia vazi linaloonekana kana kwamba lilifanana na lile la nyakati za Yesu halisi, mwana wa Mungu.

Mbali na hayo Yesu huyu alionekana amevalia viatu vyake na mkoba wake ambavyo pia viliaminika kufanana na vya yule Yesu kwenye filamu zinazosimulia hadithi ya Yesu Mtakatifu Mwana Wa Mungu.

Kulingana na watu mitandaoni walisema si vizuri kumwona mtu mwenye nywele ndefu na kumtaja kama Yesu. Pia waliongeza wakasena  Yesu huyo angekuwa mtu yeyote aliyevalia mavazi ya kuingiza.

Watazamaji wa video hiyo walipenda mshangao wa mwanamume huyo na wakashiriki utani kati yao.

 "Amerudi? Hatimaye."  @ThaboKonote alisema.

"Yesu?..kuja ubadilishe maji yawe pombe!"  Wotifaidoo alitania.

''Hili limeniacha nikiwaza, iwapo Yesu halisi angerudi kweli ningemwamini?'' Simelaneee alijiuliza.

View Comments