In Summary

• Baada ya kutua sehemu yenye vumbi, zulia jekundu lilitolewa kwa ajili ya bwana harusi na marafiki zake.

Mwanaume kwenye Ndege ya Waziri Peter Munya
Image: YOUTUBE

Mwanaume mmoja kutoka kaunti ya Kirinyaga ni gumzo kubwa baada ya kukodisha ndege aina ya helkopta kwa minajili ya kuenda ukweni kulipa mahari.

Mwanamume huyo aliyetambulika kwa jina la John Cena, alikodi chopa mbili ambazo zilimsafirisha yeye na marafiki zake hadi kwa wakwe zake kwa ajili ya hafla ya malipo ya mahari.

Baada ya kutua sehemu yenye vumbi, zulia jekundu lilitolewa kwa ajili ya bwana harusi na marafiki zake; walitembea kwa utukufu hadi kwenye ukumbi wa harusi.

John ambaye alikuwa amevalia vazi la kaki, kisha akaungana na mkewe, ambaye alikuwa ameketi kwenye kiti kama cha ufalme na kutokea kwa vazi zuri la aina yake.

Msafara huo ulizua tafrani katika kijiji hicho tulivu kwa vipaza sauti vyao huku wanakijiji wakikimbia kutazama chopa hizo.

Picha kutoka kwa hafla hiyo ya kuvutia zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mwanahabari aliyegeuka mchungaji Muthee Kiengei, ambaye alikuwa MC wa hafla hiyo. Kiengei alimpongeza rafiki yake John, akimtakia heri katika ndoa yake.

Kiengei alipakia mfululizo wa matukio hayo ndege hizo zikitua na alipoweka wazi kwamba hafla hiyo ilifanyika kwa jamii ya Agikuyu, wengi walishangaa sana kwani hawakuwa wanaamini wanajamii hao pia wangeweza kuandaa hafla kama hiyo kwani aghalabu wengi huhusisha matukio ya hadhi ya nyota tano na wanajamii wa Luo.

View Comments