In Summary
  • Mwimbaji huyo alisema tatizo hilo wakati mwingine humpata anapokuwa jukwaani hivyo kuathiri uchezaji wake
MBOSSO
Image: KWA HISANI

Mwanamuziki kutoka Tanzania Mbwana Yusuph almaarufu Mbosso amefunguka kuhusu tatizo la moyo ambalo limekuwa likimsababishia maumivu makali na kufa ganzi mikononi mwake.

Mwimbaji huyo alisema tatizo hilo wakati mwingine humpata anapokuwa jukwaani hivyo kuathiri uchezaji wake wa moja kwa moja

Akizungumza katika BBC Swahili, alisema kuwa tatizo hilo ambalo kitabibu linajulikana kwa jina la ‘arteriosclerosis’ liligunduliwa na wataalamu wa afya ambao walimweleza kuwa baadhi ya mishipa yake inayotoa damu kutoka kwenye moyo hadi kwenye viungo vya mwili imezibwa na mafuta.

“Ninapolala usiku naweza kuamka nikisikia maumivu makali hadi nalia, wakati mwingine nasikia uchungu au napata ganzi mikononi mwangu, mikono yangu inatetemeka kila wakati, nilijaribu kuwauliza wazazi wangu hivyo hivyo lakini walisema hivyondivyo jinsi ulivyozaliwa, hata ulipokuwa mkubwa ulikuwa unavunja vitu, na ndiyo maana mara nyingi nilikuwa nafanyiwa mambo mengi,” alifafanua Mbosso.

Mwimbaji huyo wa WCB  alikumbuka zaidi alipokuwa na tamasha jijini Mbeya ambapo alitakiwa kutumbuiza kwa gitaa.

Hata hivyo, muda ulipofika hakuweza kuokota gita hilo chini kwa sababu mikono yake ilikuwa ikitetemeka ilikuwa ngumu, Alibainisha kuwa meneja wake ndiye aliyechukua gitaa na kumpa.

Haya yanajiri baada ya bosso kuahirisha ziara ya kimuziki Marekani, huku akisema kwamba daktari alimwambia asisafiri kwa muda wa saa 8 kwenye ndege.

View Comments