In Summary

• Tatizo pekee ni kwamba nilifanyiwa vasektomi miaka miwili kabla ya kukutana. Anadanganya - alilia.

Image: Getty Images

Katika kizazi hiki, kuchepuka katika ndoa na mahusiano kumekuwa jambo la kawaida sana ambalo kwa bahati mbaya linafagiliwa sana na kuonewa fahari na vijana wengi pasi na kujali athari za magonjwa ya kuambukizwa zinazotokana na hulka hiyo.

Mtu yeyote ambaye ametapeliwa kimapenzi hapo awali atafahamu sana hisia hiyo ya kuumiza utakayopata mara tu unapoijua.

Ni mchanganyiko wa usaliti, maumivu makali na hasira inayochemka damu unapojaribu kuchakata habari, na kulingana na jinsi unavyoufikiria ukafiri wa mwenzako, sauti za kupiga kelele zinaweza kutokea au machozi ya kimyakimya yakadondoka.

Kuna mwanaume mmoja amezua gumzo mitandaoni baada ya kueleza jinsi mpenzi wake alichepuka na mpaka kumletea mimba akimwambia kuwa ni yake.

Kulingana na jarida la Mirro, mwanaume huyo mwenye kuvunjwa moyo alisema mpenzi wake alichepuka na kuwa alikuwa na uhakika juu ya hilo kwa asilimia mia juu ya mia, kivipi?

Mpenzi wake alikuja kususa mimba kwake, jambo lililomzuzua mwanaume wa watu kwani alikuwa anajua kuwa hawezi kupeana mimba kutokana na kuchukua mpango wa uzazi wa vasectomy.

Vasectomy ni mfumo wa kukata mishipa ya kusafirisha mbegu za kiume na hivyo mwanaume aliyefanyiwa mchakato huo hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba – lakini kwa ajabu na kushangaza, mwanadada huyu alienda nje akapata mimba na kuja kumdanganyishia mwanaume huyu kuwa mimba ni yake.

“Mpenzi wangu ametangaza kuwa ni mjamzito na ninakaribia kuwa baba. Tatizo pekee ni kwamba nilifanyiwa vasektomi miaka miwili kabla ya kukutana. Anadanganya. Ni wazi amekuwa akifanya mapenzi na mpenzi mwingine,” mwanaume huyo alinukuliwa.

Alisema kuwa kupewa taarifa za ujauzito ni dhibitisho la mashaka yake ambayo amekuwa akishuku kwa muda mrefu kuwa mpenzi wake hakuwa mwaminifu.

“Nimekuwa na mashaka yangu kwa miaka mingi. Miezi michache iliyopita, alianza kuvaa mavazi ya kifahari kazini na kuchelewa kurudi nyumbani. Wakati wa kiangazi alitangaza kuwa alikuwa na wikendi ya mazoezi na nilidhani alikuwa akienda na mpenzi wa siri. Nimevunjika moyo sana. Nilidhani huenda ndiye. Nimtoe jasho hadi lini?" aliuliza.

View Comments