In Summary

•Dorice ambaye ndiye mdogo zaidi miongoni mwa dada za Masanja alimkaribisha mtoto wake duniani hivi majuzi.

Paula Kajala na shangazi yake Dorice Masanja
Image: INSTAGRAM// DORICE MASANJA

Dada mdogo wa muigizaji wa Bongo Fridah Kajala Masanja, Dorice Masanja ameingia kwenye hatua ya kuwa mama.

Dorice ambaye ndiye mdogo zaidi miongoni mwa dada za Masanja alimkaribisha mtoto wake duniani hivi majuzi.

Mpwa wake Paula Kajala alithibitisha habari za kujifungua kwake huku akimpongeza kwa hatua hiyo maalum.

"Mama mpya zaidi mjini. Hongera 'my ride or die' @littlemap," Paula alimwandikia shangazi yake kwenye Instagram.

Watu wengine wakiwemo wanafamilia, marafiki na watu wa karibu wameendelea kumpongeza kwa hatua ya kuwa mama. Dadake Kate Masanja ni miongoni mwa waliompongeza na kumtakia kheri anapomlea mwanawe.

Dorice ni dada mdogo wa mkewe Harmonize, Kajala Masanja. Ana uhusiano wa karibu sana na bintiye Kajala, Paula.

Wakati akimsherehekea mnamo siku yake ya kuzaliwa mapema mwaka huu, Kajala alimtambua dada huyo wake kama rafiki na mshirika wake mkubwa na kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake

"Hakuna dada bora ambaye ningeweza kuota kuhusu. Wewe ni rafiki yangu mkubwa na mshirika katika uhalifu. Maisha yangekuwa magumu bila wewe. Heri ya siku ya kuzaliwa dada mdogo! Nakupenda sana," alimwandikia.

Paula pia alimsherehekea shangazi huyo wake kwa kupakia kumbukumbu yake naye. Alisema anathamini kumbukumbu zake na shangazi huyo wake  na kumshukuru kwa kuwa guzo muhimu katika maisha yake.

"Maisha ya kumbukumbu na wewe ndio hazina bora zaidi ninayoweza kuwa nayo. Asante kwa kuwepo  kila wakati na kunifundisha ukweli mwingi wa maisha haya. Unathaminiwa, nakupenda. HAPPY BIRTHDAY AUNTY,"  alisema.

View Comments