In Summary

• Sonko alikuwa amepakia picha akiwa na msanii Lavalava kwenye ofisi yake wakikagua rafu ya viatu.

Sonko akimkomesha jamaa mnoko
Image: Facebook

Katika siku za hivi karibuni, watu maarufu wamekuwa wakipitia wakati mgumu mitandaoni kutokana na kuburuzwa na wanamitandao kwa kashfa mbalimbali.

Lakini unaambiwa siku zote hakuna swali lisilo na jibu. Watu maarufu nao wamepata njia mbadala ya kuzima masimango kwa kujibu mipigo ifaavyo bila kujali nini mashabiki na wafuasi wao watawafikiria.

Juzi aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko alipakia rundo la picha kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa na msanii wa Tanzania, Lavalava. Lava alikuwa amemtembelea Sonko katika ofisi yake jijini Nairobi kutokana na maelezo kwenye picha hizo zaidi ya 20.

“Jana msanii nguli Lavalava kutoka Tanzania alinitembelea katika ofisi zangu Upper Hill Nairobi,” Mike Sonko aliandika.

Kwenye sehemu ya kutoa maoni, mtumizi mmoja wa Facebook aliyetaka kujua kama kweli hiyo ni ofisi ya Sonko ama ni duka lake la kuuza viatu, alipata jibu zito kutoka kwa Sonko.

Kuchora picha kamili, Sonko na Lavalava walionekana wakitizama rafu zilizokuwa zimejazwa viatu, jambo lililozua maoni tofauti kutoka kwa baadhi ambao walishindwa kuelewa kama ni duka ama ni ofisini mwaka kama alivyoelezea kwenye kapsheni.

Kwa utani mwingi, Sonko alimpiga kumbo mtu huyo kwa jina Kilonzo Dhe Shaddie kwa kumtania kuwa hata nguo na viatu vya mkewe ni yeye mwenyewe alimpa.

“Hata zile kanda mbili za mkeo na ile bikini, sketi ya bluu ukiongeza na suruali nyekundu unazomuona akivaa ni mimi nilimpa,” Sonko alijibu bila huruma wala kusita.

Jibu hili lilivutia vichekesho kutoka kwa watu baadhi wakisema ndio njia ya pekee kumjibu mtu anayejaribu kudadisi mambo yako ya faragha huku wengine walimsuta Sonko kuwa aliyeuliza hakuwa na ubaya.
View Comments