In Summary

• Mzee huyo alisema hataki mwanamke wa kuzaa kwa sababu hana shamba la kuwapa watoto wala pesa za kuwaelimisha.

Mzee aliyetaka mke
Image: Screengrab//Tiktok

Mchungaji Ezekiel Odero Jumapili iliyopita akihubiri katika kanisa lake kaunti ya Kilifi alistaajabishwa na mzee mmoja mkongwe ambaye aliweka ombi la ajabu kwa mchungaji huyo.

Katika video ambayo imekuwa ikisambaa mitandaoni, mzee huyo alitoa ombi kwa mchungaji Odero kuwa anataka amsaidie kupata mke mzuri mwenye umri zaidi ya miaka 50 kwani tayari wake wa awali wawili wameshafariki na kumuacha upweke.

Mwanamume huyo mwenye kichwa kilichojaa nywele nyeupe alisimulia mchungaji Ezekiel jinsi alivyokuwa ameoa wake wanne hapo awali lakini sasa hajaoa.

Zee wa watu alieleza kuwa aliwahi oa wake wawili wa kwanza ambao wote walimtoroka na kumuacha na baadae akafanya udhubutu tena wa kuoa wengine wawili ambao kwa bahati mbaya walifariki.

Alisema kuwa licha ya umri wake kwenda sana, bado hakuwa amekata tamaa katika maisha ya ndoa na ndio maana alikwenda kanisani humoili kupata msaada kutoka kwa mchungaji Ezekiel kupata mke wa 5 maishani mwake.

Kilichoshangaza wengi ni kwamba mzee huyo kinyume na wazee wengi ambao wanadakia wasichana wadogo, yeye alisema yuko tayari tu kwa mwanamke mwenye kati ya umri wa miaka 50 hadi 60 – umri ambao alisema ni wa watu waliokomaa.

Sina mke sasa hivi. Wanawake wamefika karibu wanne, wawili walienda nikafanya kuoa tena wawili wakafa. Sasa mimi niko tu, nifanyaje? Mcungaji ninataka mke mwingine lakini sitaki yule atazaa. Yesu anisaidie nipate yule amekomaa wa 52 hadi 59, huyo hazai, hana gharama kile tunapata kutoka kwa watoto tunakula naye,” mzee huyo alisimulia huku umati wa waumini wakitokwa pima machoni.

Mzee huyo alielezea sababu yake ya kutotaka yule ambaye atazaa katika kile alisema kuwa hana shamba la kuwapa watoto wengine kwani alitaka tu mtu wa kumpa kampano katika maisha ya upweke.

“Staki kupata watoto kwa sababu sina shamba la kuwagawia, sina pesa ya kupeleka watoto shule. Kwa hivyo nataka tu mama yule tunakaa pamoja tuu.”

View Comments