In Summary

•Pauline aliandikia kampuni hiyo ujumbe akiomba kusaidiwa kupata namba moja kutoka kwa laini yake ya simu  ambayo ilikuwa imefungwa.

•"Pauline, tukatae kureplace line tufunge duka? Ruka inbox, tunafaa tupange mambo 2023 sawa sawa," Safaricom ilijibu.

Image: FACEBOOK// WAMUGO PAULINE

Jibu la kitani la kampuni kubwa ya huduma za simu nchini Kenya, Safaricom kwa mwanadada mmoja ambaye aliomba usaidizi kwenye mtandao wa Facebook limekuwa likivuma kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanadada anayejitambulisha kama Wamugo Pauline kwenye Facebook aliandikia kampuni hiyo ujumbe akiomba kusaidiwa kupata namba moja kutoka kwa laini yake ya simu  ambayo ilikuwa imefungwa.

"Safaricom, nilipoteza line yangu na mumekataa kureplace😌😌 haya basi kuna kashida,🥺 mnaweza nitumia number ya mubaba nimesave Njogu Kia V8," Wamugo aliandika.

Mwanadada huyo alieleza kuwa aliitaka nambari ya 'mubaba' huyo kwa dharura kwa sababu alitapaswa kumlipia kodi.

"Landlord ashafunga nyumba hataki stori😌😌," alisema.

Mmoja wa mameneja wa kurasa za mitandao ya kijamii za kampuni hiyo aliyejitambulisha kama  FO alijibu haraka akimshauri kuripoti shida iliyomkumba kupitia DM.

Safaricom, pia kwa utani ilimfahamisha Pauline kwamba mubaba wake alikuwa na deni la mkopo wa mjazo wa simu maarufu 'Okoa jahazi.'

"Pauline, tukatae kureplace line tufunge duka? Ruka inbox, tunafaa tupange mambo 2023 sawa sawa," Safaricom ilijibu.

"Huyo Njogu pia sisi tuna mtafuta. Tunashangaa kama atalipa Okoa ama rent yako."

Mamia ya watumiaji wa mtandao walitoa maoni chini ya jibu hilo la kuchekesha huku wengine wengi wakichukua screenshot ya mazungumzo hayo mafupi na kusambaza kwenye mitandao mingine ya kijamii. 

Mazungumzo kati ya Wamugo Pauline na Safaricom
Image: FACEBOOK
View Comments