In Summary

• DCI waliwacheka kwa kuwaliwaza kuwa walishinda mabao 10 kwa saba ya Liverpool, jambo ambalo ni uongo.

DCI wakejeli United kupigwa na Liverpool.
Image: DCI// Facebook

Wapelelezi wa jinai DCI hawajaachwa nyuma katika gumzo la kejeli mitandoa kwa wapenzi wa soka ambao wanajadili matokeo ya kudhalilishwa kwa Manchester United dhidi la Liverpool usiku wa Jumapili.

Katika mechi hiyo ambayo ilifanyika ugani Anfield, Liverpool waliwadhalilisha vibaya Manchester kwa kibano cha mabao saba kappa, matokeo ambayo yamekuwa kejeli kubwa kwa United ambao wana ushabiki mkubwa haswa nchini Kenya.

Huku watu mbali mbali wakiendelea kutumia meme za kejeli kuicheka United, DCI pia hawajaachwa nyuma, na kupitia kurasa za mitandao yao ya kijamii, wamepakia picha ambayo inaonesha ubao wa mabao ukiwa umehaririwa.

Huku kila mmoja akiwa anajua United walipigwa mabao 7 kwa nunge, DCI kwenye picha hiyo walihariri kwa njia ya kejeli kuonesha kwamba United walishinda mabao 10 kwa 7 ya Liverpool, huku 10 hiyo ikiwa imehaririwa kwa kejeli na kebehi mno.

Walisema kwamba kughushi huko kwa matokeo ili kuipendelea United na kuwapa wafuasi wake nafasi ya kutabasamu ten ahata hakuwezi kuchukuliwa kama hatia katika kipengele cha katiba.

“Hatujasema hiyo 10 ni kughushi kinyume na Kifungu cha 345 cha Kanuni ya Adhabu,” DCI waliwacheka United.

Katika mechi hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi kote duniani, Wachezaji wa Liverpool Cody Gakpo, Darwin Nunez na Mohammed Salah kila mmoa alifunga mabao mawili huku Roberto Firmino alimaliza kwa bao la saba kunako dakika ya 88.

United licha ya kuwa katika fomu nzuri katika siku za hivi karibuni hadi kushinda ubingwa wa kombe la Carabao, hawakuweza kupata hata bao moja la kuvutia machozi, jambo ambalo limewageuza kucheko hata Zaidi miongoni mwa mashabiki wa soka.

 

View Comments