In Summary

•Size 8 alidokeza kwamba mahusiano yake ya awali yalikuwa yamemfanya aone kama kwamba wanaume wote ni wadanganyifu.

•DJ Mo alisema wakati alipumuona mke huyo wake mara ya kwanza alimuona kama mwenzi wake wa maisha.

Image: INSTAGRAM// SIZE 8 REBORN

Mwimbaji na mhubiri Linet Munyali almaarufu Size 8 amesema alikuwa amekatishwa tamaa na mahusiano wakati alipokutana na mume wake DJ Mo.

Akizungumza kwenye YouTube, mama huyo wa watoto wawili alisema alipokutana na DJ Mo kwa mara ya kwanza hakudhani ni mtu mkweli.

Size 8 alidokeza kwamba mahusiano yake ya awali yalikuwa yamemfanya aone kama kwamba wanaume wote ni wadanganyifu.

"Wakati huo nilikuwa napitia kipindi kibaya sana. Sikuwa naona kama niko tayari kwa mahusiano yoyote. Nilikuwa nimekatishwa tamaa sana na mahusiano. Nilikuwa naona wanaume wote ni wadanganyifu," alisema.

Msanii huyo wa zamani wa nyimbo za kuburudisha alifichua kuwa dadake ndiye aliyemshawishi kuondoa shaka na kumpa nafasi DJ Mo.

Size 8 na mcheza santuri huyo wamekuwa pamoja kwa takriban mwongo mmoja na wamebarikiwa na watoto wawili pamoja.

DJ Mo kwa upande wake alisema wakati alipumuona mke huyo wake mara ya kwanza alimuona kama mwenzi wake wa maisha.

"Mimi niliona maisha ya usoni na mtu. Sikutaka kubahatisha. Alafu nikaona vile hicho kiuno kinatingika hivyo ndiyo nitakuwa natingishiwa. Mwanaume ni kujipanga," mcheza santuri huyo alisema.

Size 8 alifichua kwamba mchekeshaji MC Jessy aliwahi kumwambia ukweli kuhusu hisia ya kwanza ya mumewe wakati alipomuona kwenye video ya wimbo wake wa kuburudisha  'Shamba Boy.'

"Jessy aliniambia DJ Mo alimwambia 'huyu msichana ni bibi yangu'. Hatukuwa tumekutana, na alisema huyo ni bibi yake," alisema.

Katika mazungumzo hayo, Size 8 alifichua kwamba huwa anasali kabla ya kushiriki mchezo wa kitandani na mumewe DJ Mo.

Mhubiri huyo alisema huwa anaomba ili apate hamu ya kufanya mapenzi wakati  mumewe anapotaka lakini hajisikii tayari.

Size 8 amefichua kwamba huwa anasali kwa Mungu kabla ya kushiriki mchezo wa kitandani na mumewe Samuel Muraya almaarufu DJ Mo. Pia alifichua kwamba kabla ya kuingia kwenye mchezo huo, yeye kawaida humwombea DJ Mo apate nguvu za kumridhisha kama ambavyo angetaka.

"Akikuja huwa namshika nasema 'Baba katika jina la Yesu' (Huwa hajui). Huwa naambia Mungu ampatie nguvu nataka kujibamba," alisema.

Mhubiri huyo alibainisha kuwa huwa anafanya maombi hayo bila ya mumewe kujua.

Size 8 aliweka wazi kwamba huwa anaomba mumewe aweze kumridhisha ili asiwahi kupatwa na fikra za kuenda nje ya ndoa.

Wakati mkewe akiendelea kufunguka ya kitandani, DJ Moh alibainisha kwamba  huwa hajui mkewe anaombea nini.

Aidha, alidokeza kuwa wakati akielekea nyumbani, pia yeye hufanya ombi kwa Mungu akimsihi awape kipindi kizuri.

"Wakati akiomba na mimi nikiwa kwa gari huwa nasema atajua mimi ni nani," alisema.

Wanandoa hao waliwashauri wapenzi wengine kumshirikisha Mungu kila wakati wanaposhiriki tendo la ndoa.

View Comments