In Summary
  • Alisema kama angekuwa anapokea mshahara mkubwa kama nyota huyo wa PSG basi angeweza kuwa na kiburi na mjeuri zaidi.
Marua amjibu Kibe
Image: Instagram

Mmoja wa watu mashuhuri wa kenya na mtayarishaji maudhui anayeishi Marekani, Andrew Kibe, amewasuta Bahati na Diana Marua kwa mara nyingine.

Kibe huwa anapinga uhusiano wao, na katika podikasti yake, kila mara hutumia bahati na Diana kama mifano.

Wakati akizungumzia suala la Hakimi, Kibe aliamua kuwahusisha Bahati na Diana kwenye hadithi hiyo, kwa kuwatumia kama mfano.

Alisema kama angekuwa anapokea mshahara mkubwa kama nyota huyo wa PSG basi angeweza kuwa na kiburi na mjeuri zaidi.

Kibe alisema kuwa jambo moja ambalo angeweza kufanya ni kuwaajiri Bahati na Diana waoshe gari lake.

Kulingana na yeye, hii ingewezekana kupitia wakala wao. Angeweza kuwalipa hadi ksh.240,000 kwa kila kipindi cha kuosha, ili kuwaonyesha kwamba yeye ni tajiri.

Alisema kwamba wanandoa wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwa hapokei mshahara mkubwa kila wiki kama Hakimi.

Hata hivyo ikiwa hilo litatokea katika siku zijazo, basi hatasita kuwaajiri wawili hao kuosha gari lake.

Zaidi ya hayo hakuna Mkenya ambaye angeweza kumwambia chochote, kwa sababu angeweza kukosa heshima ikilinganishwa na sasa.

Ijumaa kulikuwa na taarifa ambazo hazijadhibitishwa kwamba mchezaji wa kimataifa wa Morocco na timu ya PSG, Achraf Hakimi alikuwa amemrithisha mama yake mali yake yote.

Hili lilibainika baada ya mke wake raia wa Uhispania kupeleka kesi ya talaka mahakamani akidai Zaidi ya asilimia 50 ya mali ya beki huyo, lakini akapigwa na butwaa baada ya mahakama kubaini kwamba mchezaji huyo hakuwa na mali yoyote chini ya jina lake, bali mali yote yaliandikishwa kwa jina la mamake.

View Comments