In Summary

•Manzi wa Kibera alionekana akiwa ameandamana na mpenziwe kabla ya mzee huyo kupiga magoti na kumuomba wafunge ndoa.

•Watazamaji waliweza kusikika wakimsihi mwanasosholaiti huyo kumbusu mchumba wake na  wakatii amri.

Image: INSTAGRAM// MANZI WA KIBERA

Huenda tukashuhudia mwanasoshalaiti Sharifa Sharon Wambui almaarufu Manzi wa Kibera akiolewa rasmi hivi karibuni.

Jumatatu, kidosho huyo kutoka mtaa wa Kibera alichumbiwa na anayedaiwa kuwa mpenzi wake mwenye umri wa miaka 66.

Katika video zinazovuma kwenye mitandao ya kijamii, mwanasosholaiti huyo asiyepungukiwa na drama anaonekana akiwa ameandamana na mpenziwe kabla ya mzee huyo kupiga magoti na kumuomba wafunge ndoa. Makumi ya watazamaji kisha wanasikika wakimtia moyo kukubali ombi hilo la ndoa.

"Sawa, nishasema ndio!" anasikika akimwambia mpenzi huyo wake baada ya muda mfupi wa kufikiria na kuzingatia.

Baada ya kukubali, mzee huyo aliyekuwa amevalia kapura nyeupe na koti nyeusi anaonekana akimvisha pete ya uchumba.

Watazamaji wanaweza kusikika wakimsihi mwanasosholaiti huyo kumbusu mchumba wake na  wanaonekana kutii ombi.

"Kama unapenda, weka pete kwenye kidole," mwanasoshalaiti huyo alisema kwenye Instagram baada ya tukio hilo.

Katika video aliyochapisha pamoja na ujumbe huo, alionekana akijigamba kuhusu mpenzi wake na pete aliyomvisha kidoleni.

Baadaye, mwanasosholaiti huyo alidokeza kufunga pingu za maisha na mchumba huyo wake katika siku za hivi karibuni.

Katika tangazo lake Jumatatu jioni, alikejeli harusi ya mwimbaji Akothee ya hivi majuzi na kudokeza kuwa yake itakuwa kubwa zaidi.

"Harusi yangu itakuwa kubwa kuliko ucheshi huu," aliandika kwenye picha ya Akothee na mumewe siku ya harusi yao.

Hivi majuzi, mwanasoshalaiti huyo alishiriki mahojiano na mtangazaji Massawe Japanni ambapo aliweka wazi kuwa hana elimu kubwa licha ya kuwa maarufu.

Hata hivyo, alisema licha ya kutokamilisha masomo yake ya shule ya msingi ameweza kupata shahada mbili katika masomo tofauti.

"Nilisoma kidogo. Nadhani nilivukishwa shule ya chekechea nikasoma darasa la pili na la tatu. Shule ilikuwa inanichosha. Ilinichosha nikiwa katika darasa la pili la tatu hivi lakini niko na shahada," alisema.

Manzi wa Kibera ambaye alijizolea umaarufu miaka michache iliyopita alifichua kwamba, kando na kuwa na cheti ghushi cha shule ya msingi na cha shule ya upili, pia anamiliki shahada ghushi ya Ubunifu wa Usanifu na ya Rasilimali Watu.

"Ni kazi tu sijapata. Mnaninyima kazi na niko na digrii mbili?? Mnitafutie kazi," alisema.

Kidosho huyo aliweka wazi kuwa hana mpango wa kurejea shuleni kwani tayari ana mali za kumwezesha kujikimu kimaisha.

View Comments