In Summary

• Kulingana naye, alimwambia kwamba kodi ya nyumba yake ingeisha mwezi huo, na baada ya ufichuzi huo, aliacha tu kuzungumza naye na kuchimba mitini.

Mwanamke alia jamaa kumzimia data baada ya kumtongoza
Image: Twitter

Mwanamke mmoja ameshiriki na jamii nzima ya mtandao wa Twitter jinsi mvulana mmoja alivyomzimia bando chini ya saa 24 baada ya kumchumbia kwa sababu tu ya suala la kibinafsi alilomweleza kulihusu.

Akitambulishwa kama Josephine kwenye Twitter, mwanadada huyo alisema baada ya mwanamume huyo kumtupia ndoana, walikutana siku iliyofuata ili kufahamiana zaidi na ndipo walipozungumza kuhusu masuala yake ya kodi.

Kulingana naye, alimwambia kwamba kodi ya nyumba yake ingeisha mwezi huo, na baada ya ufichuzi huo, aliacha tu kuzungumza naye na kuchimba mitini.

Alibainisha kuwa hakuwahi kumwomba amlipie kodi hiyo bali alikuwa anamfahamisha tu hivyo ilishangaza kwamba aliamua kumzimia taa kutokana na kile alichokisema.

"Nilikutana na huyu jamaa jana tulizungumza nilimwambia kodi ya nyumba yangu itaisha mwezi huu na baba akaacha kuniongelesha, nilimwambia tu sikumwomba alipie," mrembo huyo alitweet.

Katika taarifa nyingine za kustaajabisha zilizosambazwa hapo awali kwenye mtandao wa Radio Jambo, mwanamume mmoja ameamua kusitisha harusi yake kama ilivyotokana na chapisho lililosambazwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kugundua jambo lisilo la kawaida kuhusu mke mtarajiwa wake.

Mwanadada huyo ndiye aliyepeleka mitandaoni akilia kwamba bwana harusi mtarajiwa alisitisha mipango yote ya harusi baada ya kugundua kwamab alikuwa amemtembelea mpenzi wake wa zamani na hata kushiriki tendo la ndoa naye usiku wote, kwa kisingizio kwamba alikuwa amempelekea kadi ya mwaliko kuhudhuria harusi.

View Comments