In Summary

• Mkwasi huyo mwenye umri wa miaka 34 alinunua jumba hilo la kifahari mwezi uliopita kwa mauzo ambayo yalivunja rekodi.

• Alinukuliwa akisema kuwa analenga kulitumia jumba hilo la thamani ya bilioni 5 kama sehemu ya kujivinjari wikendi.

Gari la kifahari likipandishwa ghorofani kwa kutumia Crane
Image: Twitter

Mwekezaji wa mali milionea ambaye alirekodiwa akiingiza gari la kifahari kwenye jumba lake la kifahari la ghorofa ya 57 amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Adrian Portelli, ambaye anajulikana kama 'Mr Lambo' kwa kupenda magari ya bei ghali, alichapisha picha kwenye Instagram siku ya Jumanne za gari hilo lenye thamani ya dola milioni 2, sawa na shilingi milioni 274 za Kenya likiinuliwa hadi kwenye jumba la upenu la dola milioni 39 sawa na shilingi za Kenya bilioni 5 na upuzi juu, huko Melbourne Mashariki.

Bw Portelli aligonga vichwa vya habari baada ya kuonekana kwenye kipindi cha The Block cha Channel Nine mwaka jana ambapo aliweka dau lililovunja rekodi kwenye nyumba hiyo iliyokarabatiwa na washiriki Omar na Oz.

Chapisho lililoelezea gari lililokuwa likipaishwa ndani ya nyumba yake kama 'mnyororo wa hali ya juu' lilizua shutuma nyingi huku kiongozi wa chama cha Greens Adam Bandt akiongoza upinzani huo.

Bw Portelli hapo awali alichapisha picha zake akiwa amepiga picha karibu na gari hilo aina ya McLaren Senna GTR katika ghorofa yake ya juu.

'Muonekano wa kwanza wa McLaren Senna GTR 57 juu. Asante sana kwa kila mtu aliyehusika kwa kufanya wakati huu wa ajabu kutokea,' aliandika.

Mkwasi huyo mwenye umri wa miaka 34 alinunua jumba hilo la kifahari mwezi uliopita kwa mauzo ambayo yalivunja rekodi ya nyumba hiyo ya bei ghali zaidi jijini humo huku akitoboka kitita cha dola milioni 39.

Walakini, anakusudia kuitumia tu kwa shughuli zake za kujivinjari wikendi.

Mfanyabiashara huyo anayejulikana kwa jina la 'Bwana Lambo' kwa kupenda magari ya michezo, aliiambia realestate.com.au aliamua kununua ghorofa siku hiyo hiyo aliyoiona kwa sababu ya 'ulinzi' na kuwa 'turubai tupu'.

View Comments