In Summary

• Prity Vishy aliandika kuwa alifanya wimbo huo bila msaada wowote ata kutoka kwa familia yake.

• Hii inamaanisha kuwa mziki huo sasa hautaweza kusikilizwa au kutazamwa na mtu yeyote katika mtandao huo.

Pritty Vish Pritty Vishy ahuzunika baada ya wimbo wake kuondolewa Youtube.
Image: Facebook

Kibao kipya cha mwana TikTok Purity vishenwa almaarufu Pritty Vishy 'Kienyeji’ umeondolewa kwenye Youtube.

Akichapisha barua kutoka kwa Youtube Prity Vishy alisikitikia hatua hiyo ya kuondoa wimbo wake kwa madai ya kuwa wimbo huo ulikiuka sheria za umiliki wa wimbo wa mtandao huo wa Youtube.

"This is not fair, mtu anisaidie, mimi ni myonge kwa sasa" alichapisha Vishy.

Mpenzi huyo wa zamani wa mwimbaji tajika, Stevo Simple Boy alikuwa ameachilia wimbo huo siku ya Jumatano na wimbo huo haukuwa umemaliza hata siku moja kabla ya kuondolewa.

Prity Vishy aliandika kuwa alifanya wimbo huo bila msaada wowote ata kutoka kwa familia yake.

“Nafanya vitu zangu, hakuna msaada kutoka ka familia yangu alafu naamka napata mtu amenifanyia hivi ”

Barua hiyo ilisema kuwa kwa sababu ya ukiukaji wa sheria ya umiliki wa wimbo wake walilazimika kuuondoa kutoka Youtube.

"Due to copyright takedown notice that we received, we had to take down your video from youtube" ilisoma sehemu ya taarifa hiyo.

Hii inamaanisha kuwa wimbo huo sasa hautaweza kusikilizwa au kutazamwa na mtu yeyote katika mtandao huo.

Pritty vishy hivi majuzi alijitokeza na kumtambulisha mpenzi wake mpya anayeishi Marekani Dj Starvy ambaye wamekuwa marafiki kwa muda sasa kabla ya kuamua kuingia katika mahusiano ya kimapenzi.

Pritty vishy aliingia kwenye mahusiano na mcheza santuri huyo baada ya kutengana na  Stivo simple Boy.

Kulingana na Pritty Vishy wawili hao waliachana kwa kuwa alihisi Stevo hakuwa anamtetea dhidi ya jamaa zake. 

View Comments