In Summary

• Manzi wa Kibera Jumanne alichapisha picha wakiwa kwenye harusi baada ya kurudiana na mzee huyo siku tatu zilizopita.

• Wawili hao walikuwa wametengana mwezi Mei baada ya Manzi wa Kibera kutangaza kwenye akaunti yake ya Instagram kuwa hawako kwenye mahusino tena.

Manzi wa kibera kwenye harusi yake na Nicholas Kioko.
Image: INSTAGRAM/ MANZI WA KIBERA

Mwanasoshalaiti Sharifa Sharon Wambui almaarufu Manzi wa Kibera amefunga ndoa na mpenzi wake mzee, Nicholas Kioko.

Manzi wa Kibera Jumanne alichapisha picha wakiwa kwenye harusi baada ya kurudiana na mzee huyo mwishoni mwa juma lililopita.

“It doesn’t who you love as long as you are happy”  Manzi wa kibera aliandika katika picha aliyochapisha wakiwa wamevishwa pete ya harusi.

Licha ya kuchumbiana kwa muda mrefu, kipusa huyo anayezungukwa na sarakasi nyingi maishani alibainisha kwamba anasubiri ndoa rasmi ili kumuonjesha mchumba huyo wake zawadi ya ndoa aliyomhifadhia, sasa mashabiki wake walifurahia mzee atapokea zawadi yake baada ya kuhalalisha ndoa yao.

"Mpaka tufunge ndoa ndio tutafanya tendo hilo." Manzi wa Kibera alijibu swali la shabiki mmoja aliyemuuliza mpenzi wake hudumu masaa mangapi kitandani.

Wawili hao walikuwa wametengana mwezi Mei baada ya Manzi wa Kibera kutangaza kwenye akaunti yake ya Instagram kuwa hawako kwenye mahusino tena.

Mwanasoshalaiti huyo alielezea kuwa amewaza kuvunja mahusiano na mpenzi huyo wake wa miaka 66 kutokana na chuki na unyanyasaji iliyoko mtandaoni.

Jumatano, Juni 6 Mzee huyo alijitokeza na kutaka kurudishiwa Hati miliki ya shamba lake alilompea Manzi wa Kibera amuekee salama.

Katika mahojiano hayo na runinga moja ya mitandaoni Mzee huyo alikiri kuwa bado alikuwa anampenda binti huyo kutoka mtaa wa mabanda wa Kibera na angependa warudiane.

"Akileta hiyo na aniambie tuko pamoja nitakua sawa. Na yeye anipende kama vile nilikua nampenda mbeleni tukimaliza hiyo tupange harusi," Nicholas alisema.

Kwa hakika maombi yake yamejibiwa na sasa wameingia katika ndoa na mpenzi wake.

View Comments