In Summary
  • Ingawa hakuwahi kutaja waziwazi mapenzi ya maisha yake DJ Fatxo, aliweka wazi kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwamba yeye na mtoto walimpenda kweli.
DJ FATXO NA MPENZIWE GATHONI
Image: KWA HISANI

Gathoni Waruguru, mpenzi wa mwimbaji mashuhuri wa Mugithi DJ Fatxo amedokeza kuwa kwa sasa ana ujauzito wa mtoto wake.

Malkia huyo ambaye pia ni mtangazaji katika kituo cha runinga cha Nyumba Ituu alidokeza haya katika chapisho lake la hivi punde kwenye akaunti yake ya Instagram, ambapo aliandika ujumbe akisherehekea babake mtoto katika Siku ya akina Baba duniani.

Ingawa hakuwahi kutaja waziwazi mapenzi ya maisha yake DJ Fatxo, aliweka wazi kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwamba yeye na mtoto walimpenda kweli.

Pia alisindikiza ujumbe huo kwa emoji ya mama aliyembeba mtoto.

"HAPPY FATHER'S DAY TO MY BABY DADDY ❤️...TUNAKUPENDA 👨‍🍼 🥺".

Gathoni Waruguru na DJ Fatxo hata hivyo wamekuwa wapenzi kwa muda sasa, ingawa uhusiano wao ulijulikana kwa umma mapema mwaka huu.

Tangu wakati huo wapenzi hao wamekuwa wakionyesha malengo yao ya kuvutia kwa mashabiki wao.

Hii ni kupitia picha nzuri ambazo huwa wanachapisha wao kwa wao, na pia maneno matamu ambayo huwa wanaandikiana kwenye mitandao ya kijamii.

 

 

 

 

 

View Comments