In Summary

•Baadhi ya mashabiki wamedai kuwa mwimbaji Samuel Muchoki almaarufu Samidoh ndiye aliyemshambulia seneta Nyamu.

•Nyamu alikanusha tetesi za mitandaoni kwamba jicho lake jeusi lililoonekana kwenye picha iliyosambaa mitandaoni lilitokana na unyanyasaji wa kinyumbani.

Seneta Karen Nyamu alionekana na michibuko usoni
Image: HISANI

Seneta Karen Nyamu ameendelea kukanusha madai ya unyanyasaji wa kinyumbani kufuatia wasiwasi ulioibuliwa baada ya kuonekana hadharani akiwa na michibuko usoni.

Hivi majuzi, kumekuwa na madai kwamba mama huyo wa watoto watatu huenda alipigwa na mpenzi wake, kitendo kilichomuacha na michibuko karibu na jicho lake. Baadhi ya mashabiki hata wamedai kuwa baba wa watoto wake wawili, mwimbaji Samuel Muchoki almaarufu Samidoh ndiye aliyemshambulia, madai ambayo seneta huyo wa UDA amejibu.

Kwenye mtandao wa Facebook, shabiki mmoja alimwandikia, “Walisema eti umechapwa na Samidoh.”

Nyamu ambaye anajulikana kuwa mbishi sana katika majibu yake kwa wanamitandao alisema, "Na tarimbo."

Mtumiaji mwingine wa Facebook aliandika “Washow wewe labda uchapwo na Dickson Munene, my favourite.”

Alijibu, "Wanajifanya hawajui."

Jumapili jioni, seneta Nyamu alikanusha tetesi za mitandaoni kwamba jicho lake jeusi lililoonekana kwenye picha iliyosambaa mitandaoni lilitokana na unyanyasaji wa kinyumbani.

"Mnajua mimi si mtu wa kujali wanachosema kuhusu maisha yangu binafsi au chochote kile. Chochote unachotaka kusema juu yangu unajua inakuanga bure. Sicatch, sijali kwani sina issue kabisa. Kwa kweli saa zile hamniongelei nakuangaa na wasiwasi kidogo."

Karen Nyamu aliwahutubia wanamitandao katika kipindi cha moja kwa moja kwenye mtandao wa Facebook ambapo alijibu wasiwasi kuhusu jicho lake na kufunguka kuhusu changamoto anayokabiliana nayo.

Katika video ya dakika 10, Karen aliendelea. "Lakini kuna jambo ambalo limenivutia. Ni picha ambayo tulipiga siku ya Ijumaa kwenye hafla moja huko Nyeri katika Ofisi ya Skauti na Girl Guides ambapo spika wa Seneti alikuwa mgeni mkuu katika hafla ya kufunga na hivyo tulikuwa tumeandamana na yeye na maseneta kadhaa na hii picha nimepigwa imefunika macho yangu moja, whatever alafu sijui kuna nini.

Kwa hiyo watu wanakejeli unyanyasaji wa kijinsia hasa watu wale hawanilike, wanafikiri ukatili wa kijinsia ni kitu ambacho unaweza kukitumia kujibu mzozo au kitu ambacho unapaswa kuwatakia maadui zako na hawa ni wanawake. Hatuwezi kuwa wajinga hivi katika zama hizi. Unyanyasaji wa kijinsia ni suala zito, unaathiri asilimia 40 ya wanawake nchini Kenya kama vile Afrika unavyoathiri wanawake zaidi kuliko wanaume."

Alisisitiza hakuna mtu aliyempiga, na hapakuwa na jicho jeusi.

View Comments