In Summary
  • Grace, mke wa rapa huyo alisema alijisikia vibaya mumewe alipolazimishwa kuwapigia debe wanawake hao.
Mwanamuziki Stivo Simple Boy
Image: HISANI

Rapa Stevo Simple Boy, anasema alilazimika kutafuta kikib sana  wakati aliposajiliwa chini ya lebo ya rekodi ya Men In Business (MIB).

Mwimbaji huyo alisema kuwa hapendi kutafuta kiki iliohusisha wanawake wengine kwani yeye ameoa.

"Sikuwa sawa na kiki, nililazimika kufanya hivyo. Uliponiona na magari ya kifahari, hiyo ilikuwa biashara lakini ilifika mahali meneja alipanga kiki na wanawake."

 

Kwa sababu nina mke, kwa nini waweke wanawake wengine kwenye ukurasa wangu na kusema uongo kwamba ninawatamani?"

Grace, mke wa rapa huyo alisema alijisikia vibaya mumewe alipolazimishwa kuwapigia debe wanawake hao.

"Nilimwambia meneja kuwa anachofanya si kizuri na hakuweza kunisikiliza."

Stevo alisema atapata 30% ya pesa alizofanyia kazi, huku lebo hiyo ikichukua 70%. Mwanzoni, alikuwa akiishi katika nyumba ya Ksh 7K huko Utawala na alihamishwa hadi nyumba ya vyumba viwili vya kulala ya 10K.

“Video zangu zilikuwa zikishutiwa na wasamaria wema lakini bado uongozi ungepata zile asilimia 70. Lakini sababu kubwa iliyonifanya niondoke kwenye lebo hiyo ni kwa sababu meneja na mke wangu hawakuwa na maelewano mazuri, kuna mambo mke wangu alihisi hayaendi sawa. lakini meneja hakumsikiliza."

Katika taarifa yao, MIB walisema wamempa rapper huyo siku 35 za mabadiliko mazuri.

"Tunapenda kukutaarifu kuwa hatutaki tena kuendelea na mkataba wetu wa muziki na wewe. Barua hii ni taarifa kwako nia yetu ya kusitisha mkataba huo kwa njia halali na kwa mujibu wa itifaki," ilisomeka sehemu ya barua

 

"Kukomeshwa kwa mkataba kutaanza tarehe 31 Julai kwa hivyo tuna siku 35 za kuwasilisha maslahi ya pande zote mbili kwa ajili ya mabadiliko ya haraka. Wakati wa mchakato huo, wahusika wote watasitishwa na mchakato halali wa matukio utafuatwa kulingana."

Barua hiyo inaisha kwa kumshukuru mwimbaji huyo kwa ushirikiano wake wakati wa mkataba wake "Tafadhali usisite kuwasiliana."

View Comments