In Summary

•Zari Hassan alidaiwa kumuita mumewe Shakib Cham Lutaaya 'fala' katika sauti ya mazugumzo ya simu iliyosambaa.

•Baada ya sauti hiyo kusambaa, Shakib alijibu kwa njia isiyo ya moja kwa moja akidokeza jinsi alivyosikitoshwa na matamshi ya mkewe.

Zari Hassan, GK Choppa, Shakib Cham
Image: HISANI

Wiki jana, kulikuwa na mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya mwanasosholaiti wa Uganda, Zari Hassan kudaiwa kumuita mumewe Shakib Cham Lutaaya 'fala' katika sauti ya mazugumzo ya simu iliyosambaa.

Katika sauti hiyo ambayo inadaiwa kuwekwa hadharani na promota aliyetofautiana na Zari, mama huyo wa watoto watano alisikika akizungumzia jinsi mumewe mwenye umri wa miaka 31 anavyokosa kujiamini na ambavyo hajui lolote.

Wanamitandao walikuwa wepesi kumkosoa mpenzi huyo wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz kwa matamshi yake huku baadhi wakionekana kumshauri Shakib kufuatia aibu hiyo ya umma. Mmoja wa wapenzi wa zamani wa Zari, GK Choppa ni miongoni mwa waliotoa ujumbe wa kejeli kufuatia sauti hiyo.

"Ujumbe kwa wale wote wanaotaka kuwa kama Choppa, pata pesa na uepuke kuwa fala ... na ufurahie maisha kikamilifu, na uende na sheria zako mwenyewe, kusema tu," GK Choppa alisema kupitia mtandao wa Instagram.

Zari Hassan na mfanyibiashara GK Choppa walichumbiana kwa muda mfupi mapema mwaka jana kabla ya kutengana kwa njia ya kutatanisha. Katika kipindi cha uchumba wao, Waganda hao wawili walionekana wakibarizi na kufurahia nyakati pamoja.

Mwanasholaiti huyo mwenye umri wa miaka 42 alijitosa kwenye mahusiano na Shakib Cham muda mfupi tu baada ya kuachana na Choppa. Katika mazungumzo ya simu yaliyovunjishwa wiki jana, Zari alisikika akimwagiza mtu aliyekuwa akizungumza naye atoe maelezo ya kina kwa mumewe huku akieleza kuwa hajazunguka dunia sana na anahitaji taarifa za wazi kuhusu nini kinatarajiwa juu yake.

“Ebu mpe briefing, mpe briefing. The only international trip amewahi kufanya Dubai na Dubai they are not so strict at the airport. Hiyo ya UK, hata kama uko na kila kitu wanauliza. Unahitaji kumpa maelezo mafupi,” Zari alisikika akisema kwenye sauti hiyo kabla ya kutoa maelezo zaidi kwa lugha ya Kiganda.

Aliendelea, “Unajua Shakib anapanic. Ni insecure hivyo. Kuingia kwenye counter hivyo mtu kumuuliza maswali na kuanza kujibu, anapanic. Yeye mwenyewe hajiamini vile alivyo, hajiamini. Anaanza kusema vitu vyake.”

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz alisikika akitoa maelekezo zaidi kwa mtu aliyekuwa akiongea naye kwa lugha ya Kiganda.

 “Mume wangu hajiamini. Kwanza kabisa, anakuanga na haya, anaanza kuogopa, anapanic..,” Zari alisema kabla ya kuendelea zaidi kumwita kijana huyo wa miaka 31 ‘fala’.

 “Kwa upole wake hapo ndio nampendea, yeye ni fala,” aliongeza.

Baada ya sauti hiyo kusambaa, Shakib alijibu kwa njia isiyo ya moja kwa moja akidokeza jinsi alivyosikitoshwa na matamshi ya mkewe.

“Usiongee vibaya kuhusu mume wako kwa mtu yeyote… Niheshimu nisipokuwepo. Hiyo ndiyo ninayouliza, " Shakib alisema kwenye mtandao wa Facebook .

Mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 31 pia alizungumza kuhusu jinsi kiburi kinaweza kumfanya mtu kupoteza kitu kizuri.

"Mapenzi yatakufanya uonekane mjinga. Lakini kiburi kinaweza kukufanya ukakosa kitu ambacho hutapata tena,” alisema Shakib.

View Comments