In Summary

• Mchungaji Ezekiel Odero amedai kuwa kumpata mwanamume mjaluo ambaye bado ni mwaminifu kwa mke wake ni tukio adimu sana katika jamii hiyo. 

 

Mchungaji Ezekiel Odero.
Image: MAKTABA

Mchungaji Ezekiel Odero amedai kuwa kumpata mwanamume mjaluo ambaye bado ni mwaminifu kwa mke wake ni tukio adimu sana katika jamii hiyo. 

Katika video moja iliyokuwa ikienea katika mtandao wa TikTok, Pasta Ezekiel alielezea hisia zake na waumini wa kanisa lake la New Life Prayer Centre kule Mavueni Kilifi alifichua kuwa si rahisi kupatikana kwa mwanaume mwaminifu katika jamii ya Waluo.

“Ukipata mwanaume mwaminifu ujaluoni kwa mke wake, shukuru Mungu ameshuka asubuhi. Mwanaume mjaluo haoni skirt ikipita akaacha. Ni ukweli lakini haoni skirt ikipita.”

Mchungaji huyo anayekabiliwa na kesi mahakani, aliwasifia wanaume hawa, ambao kulingana naye wanafahamu njia za kuwaonyesha mapenzi ya dhati wanawake wao. 

“Ukienda sehemu za ujaluoni watu wanapenda wake zao sana, anapenda mke wake sana anaeza mnunulia hata radio inatoshana na nyumba. Lakini anamwambia we nini iko sumbua wewe. Wewe iko na radio kubwa baby wewe tulia baby.”

Mchungaji Ezekiel anafahamika kote nchini kwa mahubiri yake ya kufunza na kuwaonya Wakenya kwa jumla kughura dhambi na kutafuta uso wa Bwana Yesu. Lakini hivi majuzi amekuwa akichunguzwa kwa miongoni mwa makosa mengine mafunzo ya itikadi kali na ulanguzi wa fedha lakini bado hajafunguliwa mashtaka kwa kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu madai hayo.

Mwezi uliopita serikali ilighairi mikutano iliyokuwa imepangwa na mhubiri huyo huko Machakos na Nairobi lakini siku ya Jumamosi na Jumapili aliweza kuwa na mkutano wa hadhara katika uwanja wa Jacaranda jijini Nairobi.

View Comments