In Summary

•Milly WaJesus amewashauri wanawake kufanya mapenzi na waume zao angalau mara tatu kwa siku ili ngozi zao zing'ae.

•Mama huyo wa watoto wawili alidokeza kuwa ratiba hiyo ya mapenzi pia husaidia kupunguza viwango vya msongo wa mawazo.

Kabi WaJesus na mkewe Milly WaJesus
Image: INSTAGRAM

Mwanavlogu mashuhuri Millicent Wambui almaarufu Milly WaJesus amewashauri wanawake kufanya mapenzi na waume zao angalau mara tatu kwa siku ili ngozi zao zing'ae.

Katika taarifa yake kwenye Threads muda mfupi baada ya kujiunga na mtandao huo mpya wa kijamii siku ya Alhamisi, mama huyo wa watoto wawili alidokeza kwamba ratiba hiyo ya mapenzi pia husaidia kupunguza viwango vya msongo wa mawazo.

Milly alibainisha kuwa kufuata ratiba hiyo kumemsaidia sana baada ya yeye na mumewe Peter Kabi almaarufu Kabi WaJesus kuamua kujaribu.

"Inaonekana kufanya mapenzi na MUMEO mara tatu kwa siku hufanya ngozi yako ing'ae na kupunguza viwango vyako vya msongo wa mawazo. Nimefurahi kuwa nimeijaribu na inanifanyia kazi,” Milly WaJesus alisema na kuambatanisha ujumbe wake na picha inayoonyesha uso wake ukiwa umeng'aa.

Aliongeza, “Watu single fanyeni tu skincare routine badala yake. Je, kuna dawa tena ya afya na ngozi inayong'aa?

Mwanavlogu huyo mwenye umri wa miaka 29 aliwashauri wanawake wote walioolewa wajaribu utaratibu wa kufanya mapenzi mara tatu kwa siku ikiwa taratibu nyingine za matibabu ya ngozi yao hazijaleta matokeo.

Kabi na Milly ni kati ya wanandoa maarufu zaidi kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya. Wawili hao mara nyingi huonyeshana upendo na usaidizi wao kwa kila mmoja hadharani katika juhudi za kuwatia moyo watu wengine walio kwenye ndoa.

Mwezi Desemba mwaka jana, wanandoa hao Kabi waliadhimisha miaka mitano tangu walipofunga pingu za maisha.

Wawili hao walifanya harusi ya kanisa mnamo Desemba 2, 2017 na wamekuwa wakiishi vizuri kama wanandoa kwa miaka mitano iliyopita.

Wakati wakiadhimisha hatua hiyo kubwa, Milly alibainisha kuwa kukubali kujitosa kwenye ndoa na mume huyo wake ndio uamuzi bora zaidi ambao amewahi kufanya maishani.

"Abebo wangu 😍. Kusema nataka kushiriki maisha yangu yote na wewe ulikuwa uamuzi bora zaidi ambao nimewahi kufanya. Ninakupenda zaidi kila siku," Milly alimwambia Kabi kwenye mtandao wa Instagram.

Katika chapisho lingine, Milly alimtambua mumewe kama rafiki wake mkubwa, mshirika wa biashara, mhubiri na baba bora wa watoto wao. Aidha, alimhakikishia Kabi kuhusu mapenzi yake makubwa kwake.

View Comments