In Summary

•Mwimbaji huyo wa Mugithi amedokeza kuwa bado ana umri mdogo sana kufikia kuitwa ‘mubaba’.

•Uchumba wa Samidoh na Karen Nyamu umezalisha watoto wawili huku pia akiwa na watoto wengine watatu na Edday Nderitu.

Karen Nyamu, Samidoh, Edday Nderitu
Image: INSTAGRAM

Mahusiano ya mwimbaji wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh ni mojawapo ya yale yanayojadiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya.

Mwanamuziki huyo anayeimba kwa lugha ya Kikuyu anaaminika kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu. Pia amekuwa kwenye ndoa ya muda mrefu na Bi Edday Nderitu kwa zaidi ya muongo mmoja.

Siku ya Jumatatu, mtumiaji wa Facebook alitoa maoni kwenye moja ya machapisho yake akimuita "Mubaba wa Karenzo (Karen Nyamu) na Edday."

Samidoh ambaye anajulika kupenda sana kujibizana na mashabiki wake kwenye akaunti zake tofauti za mitandao ya kijamii hata hivyo alionekana kupinga jina hilo alilopewa na mtumiaji huyo wa mitandao ya kijamii.

Katika jibu lake, mwanamuziki huyo kutoka Kaunti ya Nyandarua alidokeza kuwa bado ana umri mdogo sana kufikia kuitwa ‘mubaba’.

“Mimi mtoto mdogo tu, one man guitar nimefika miaka ya kuitwa mbabaz?,” Samidoh alijibu.

Uchumba wa mwanamuziki huyo na Karen Nyamu kwa muda usiojulikana umezalisha watoto wawili, msichana na mvulana huku pia akiwa na watoto wengine watatu na mke wake wa muda mrefu Edday Nderitu.

Image: FACEBOOK// SAMIDOH

Mapema mwezi huu, seneta Nyamu alibainisha kuwa ni maombi yake kwamba mpenzi wake Samidoh atakuja kuungana tena na familia yake na Edday Nderitu ambayo imekuwa ikifurahia muda nchini Marekani.

Wakili huyo alithibitisha kuwa ni maombi yake kuwa siku moja Edday atarudi nyumbani ili wawe familia moja kubwa.

Nyamu alikuwa amechapisha nukuu kuhusu kuwasaidia wengine wakati mke huyo wa mzazi mwenzake alipofanywa kuwa mada.

"Kumbuka wakati wowote unapokuwa katika nafasi ya kusaidia mtu, furahiya kufanya hivyo kila wakati kwa sababu huyo ni Mungu anayejibu maombi ya mtu mwingine kupitia wewe," Karen Nyamu aliandika kwenye mtandao wa Facebook siku ya Jumapili.

Shabiki mmoja alijibu, "Siku moja familia ya Edday itaungana tena."

Bila kusita, seneta Nyamu alionekana kukubaliana na maoni ya shabiki huyo na wakati huo akadokeza kwamba angefurahi sana kuona familia ya Muchoki ikiungana na kuwa kubwa tena.

“Ni maombi yetu pia. Tukue familia moja kubwa.”

Katika maoni mengine, shabiki alimuuliza jinsi alivyokuwa akimsaidia mke huyo wa Samidoh kujibu maombi yake.

‘Nashangaa ni maombi gani ya (Edday) ambayo Mungu anajibu kupitia wewe,” Mtumiaji wa Facebook aliuliza.

Karen alijibu, “Mungu atatumia watu wengine kuniamini.

View Comments