In Summary

• Anasema haitaji watoto zaidi wala hataki kuoana na mtu wa nje na baadhi ya watu wa familia zao wanaweza kutengwa.

• Mkewe alimuacha na watoto watatu, wavulana wawili na msichana mmoja.

NDOA: Jamaa ataka kumuoa mama mkwe baada ya kifo cha mkewe.
Image: FACEBOOK

Kisa cha mwanamume kutoa pendekezo la kumuoa mama mkwe baada ya mkewe kufariki dunia kimevutia hisia mseto mitandaoni.

Katika hadithi iliyochapishwa kwenye Facebook na mtumizi mmoja wa mtandao huo wa Meta, Azuka Onwuka, mwanamume huyo alisema ni bora kuoa mama mkwe na kuepuka mtu wa nje ambaye kwa namna moja au nyingine anaweza kuwatesa watoto ambao mkewe – binti wa mke mtarajiwa – aliacha.

Mke wa mtu huyo alifariki akiwa na umri wa miaka 34, na kuacha watoto watatu, wavulana 2 na msichana. Mwanamume huyo, ambaye sasa ana umri wa miaka 46 anapendekeza kuoa mama mkwe wake, ambaye ni mjane mwenye umri wa miaka 57.

Ingawa pendekezo la ndoa limezua hisia, mwanamume anasisitiza kwamba ndivyo anataka na kwamba tayari ameshapata hisia kwa mama mkwe.

Alisema kwamba kwa kumuoa mama mkwe, ni kama njia moja ya kuhakikisha malezo bora yasiyo na ubaguzi kwa wanawe na pili ni kama kumsitiri mama mkwe ambaye mumewe alifariki muda mrefu nyuma na kumuacha mjane.

 Hadithi hiyo inasomeka hivi:

 "Mwanamume (jina linahifadhiwa) alifiwa na mke wake baada ya kupata watoto watatu (wavulana wawili na msichana). Mkewe alikufa akiwa na umri wa miaka 34. Miaka miwili baadaye, anataka kuoa mama mkwe wake ambaye ana umri wa miaka 57 na mjane. Ana umri wa miaka 46. Anasema haitaji watoto zaidi wala hataki kuoana na mtu wa nje na baadhi ya watu wa familia zao wanaweza kutengwa na familia nyingi ambazo zinaweza kutengwa."

Je, kuna mila zinazokubali ndoa ya aina hii?
View Comments