In Summary

•Bahati alikuwa akiiga jinsi mwanamume huwa anahisi wakati mwanamke anapomwomba amshikie mkoba wake.

•Bahati alionekana akiwa amevalia gauni jekundu, hereni, lipstick kwenye midomo na wigi kichwani

Image: INSTAGRAM// BAHATI

Mwimbaji Kelvin Kioko almaarufu Bahati amewajibu kwa kejeli wakosoaji wake baada ya kukosolewa vikali kwa kuvaa mavazi ya kike na kujipaka vipondozi ili kuigiza mchezo wa ya burudani na mkewe Diana Marua.

Katika video ya hivi majuzi iliyochapishwa kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii, Bahati alionekana akiwa amevalia gauni jekundu, hereni, lipstick kwenye midomo na akiwa wigi kichwani. Alikuwa akiiga jinsi mwanamume huwa anahisi wakati mwanamke anapomwomba amshikie mkoba wake.

“Wanadada, hivi ndivyo mwanaume unavyojisikia unapompa mkoba wako akushikie. Aki babe (Diana) wacha kila mtu ajibebee vitu vyake aarg,” Bahati aliandika kwenye maelezo ya video hiyo iliyochapishwa  siku ya Jumanne.

Video hiyo ilizua hisia mseto kutoka kwa wanamitandao, baadhi wakiwapongeza wanandoa hao kwa muungano wao mzuri huku wengine wakiwakosoa kwa kitendo hicho.

Huku akiwajibu wakosoaji, mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili alibainisha kuwa baadhi ya wanaume wanamkosoa ilhali anaonekana mrembo kuliko wapenzi wao wa kike.

“Unaongea mbaya na nimeiva kuliko Dem yako,” Bahati alisema siku ya Jumatano kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha yake akiwa amevalia gauni nyekundu, wigi na vipodozi usoni kuonyesha kuwa anajivunia hilo.

Mwimbaji wa nyimbo za injili Ringtone Apoko ni miongoni mwa watu ambao hawakuchelewa kumkosoa Bahati kwa kuvaa mavazi ya kike.

“Kweli kabisa hii ni nini??? Ni nini hawa kutoka kwa wanamuziki wa kiume wa Kenya,” Ringtone alionekana kushangaa.

Tazama maoni mengine kutoka kwa baadhi ya wanamitandao Wakenya;

@nancyakinyi955 Nyinyi sasa ndio mnafaa kutupreachia mambo ya marriage works.

official.kakajay Bahati anahitaji manager juu huyu sio Bahati wazami

brendajadoc it's the tongue roll for me

k.hurney he was loving the woman he has become

harriet_njeru ati mbunge mtarajiwa, we are joking as a country

truppacreations Hiyo miguu ya baha iko na kiu ya mafuta

View Comments