In Summary

• Video hiyo ilizua maswali kuhusu maisha ya kila siku ya mwanamume huyo, jinsi anavyofanya kazi akiwa na kucha hizo ndefu na motisha ya uamuzi wake wa kuzifuga kwa muda mrefu.

Mwanume kutoka Mombasa mwenye kucha ndefu.
Image: INSTAGRAM

Hisia mseto zimeibuka mitandaoni baada ya mwanaume mmoja anayefahamika kama John Waweru kuibuka na kuonyesha kucha zake ndefu ambazo alikiri kuwa amekuwa akizilea kwa zaidi ya miaka 22.

Video ya kustaajabisha iliyochapishwa mitandaoni ilimnasa mwanamume huyo wa Mombasa  akionyesha kucha zake ndefu zilizopakwa rangi za bendera ya Kenya, kila kucha ikionekana kuwa ndefu kuliko nyingine.

Video hiyo ilizua maswali kuhusu maisha ya kila siku ya mwanamume huyo, jinsi anavyofanya kazi akiwa na kucha hizo ndefu na motisha ya uamuzi wake wa kuzifulea kwa muda mrefu.

Waweru katika mahojiano  na runinga ya Ebru mwaka wa 2019 alikanusha madai ya wakazi wa Mombasa waliohusisha hatua yake ya kulea kucha na uchawi akieleza kuwa yeye hufanya kazi zake bila matatizo yoyote kwani alikuwa ashazoea kucha zake ndefu.

"Hizi si za uchawi, nimezoea kukaa tu nazo na sioni kama ni ngumu kufanya kazi zangu. Hizi kucha ninazipenda sana siezi na sitawai kuzikata."

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 40 alifichua kuwa alikuwa akifanya kazi ya kulipisha wakaazi wa Mombasa katika ufuo wa bahari ya hindi na shuleni anapoalikwa. Hela hizo zimeweza kumsaidia kununua kila kitu anyomiliki nyumbani kwake.

"Hizi kucha unaona hapa zinanilipia kodi ya nyumba na hizi vitu zote unaona kwa hii nyumba ni pesa ya hizi kucha."

Wanamitandao walishangazwa na kuelezea wasiwasi wao na hizi hapa baadhi ya maoni yao;

mulamwah : Anazichunga usiku kucha

___daddyz : We blame Ruto button

robinrookc__sharia.a :How does he even remove his trouser

kafuri_fx : Si mchill ata nimee ndevu buana

thee_nairobi_kid : Hapo kwa choo is where we draw the line

trending_teen_254_ : Alafu nikisema atoe horror movie. Kenyans will judge me,anyways Eric asione hii atavaa sengenge

dote___ : Huyu akienda choo huwa hajipanguzi

ruiru_kiddoh_ : Dah ,,,,,,,,😂kumamake ana mikucha mirefu😂

lenny_vybzz: Sasa huyu akienda Choo....ama Acha tu

_tonimali : Na mimi hapa nakula zangu ju ya njaa 😂

View Comments