In Summary
  • Baba huyo wa watoto watatu alisema yeye ni mfanyabiashara halali.
  • Katika mahojiano na Mungai Eve, Rapudo anasema yuko sawa na kile anachotengeneza.
Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Amber Ray amekuwa akimshinikiza babake mtoto  wake na mpenziwe Kennedy Rapudo kujiunga na siasa za Kenya.

Katika mahojiano na Mungai Eve, Rapudo anasema yuko sawa na kile anachotengeneza.

"Kila mara anataka nijiunge na siasa lakini sio kikombe changu cha chai.Watu wanakwenda kutafuta pesa na wengi wao wanapata kupitia rushwa.

Nyingi ni kutokana na ufisadi, ninachotengeneza kinatosha kwa familia yetu. Siasa za Kenya ni mchezo mchafu sana.

Ikiwa mambo yatabadilika katika siku zijazo labda ndio, lakini kwa sasa acha niendelee kuendesha biashara zangu."

Amber Ray alitoa sababu zake za kutaka mpenziwe ajiunge na siasa.

"Una moyo mzuri na mkubwa na watu wanahitaji hivyo, watu wanahitaji aina tofauti ya siasa, unaweza kusaidia watu wengi.

Mambo yanabadilika."

Rapudo pia alizungumzia madai kuwa anajihusisha na biashara ya Wash Wash.

Baba huyo wa watoto watatu alisema yeye ni mfanyabiashara halali.

"Watu wamekuja na nadharia nyingi ikiwa ni pamoja na kwamba mimi ni mtu wa kuosha.

Huwezi kuniona na Wash Wash guys, naishi maisha safi.

Sipendezwi na Wash Wash.Sitaki kuishi maisha ambayo ni lazima niishi maisha ambayo ninatazamwa.

Osha Osha sio kikombe changu cha chai.

Marafiki na familia yangu wanajua biashara yangu lakini kwa sasa, napendelea kuifanya iwe ya faragha. Ikiwa nitawahi kugombea kiti cha kisiasa ningewaambia watu ninachofanya."

Wawili hao, wakizungumza na runinga ya mitandaoni ya SPM BUZZ wakati wa hafla ya kufahamu jinsia ya mtoto wa Eric Omondi, waliwaeleza wafuasi kuwa wanapanga kuondoka Kenya kabisa.

"Tumekuwa tukifikiria kwa sana na sioni tukiishi Kenya hivi karibuni. Tunapanga kuondoka na kuhamia nchi nyigine. Hamuezi jua tutaondoka na privat jet kwa sababu nafanya kazi kwa bidii na pia mke wangu anataka pirivate jet. so…"

Mfanyibiashara huyo aliongeza kuwa sababu ya mahusiano yake na Amber Ray kudumu kwa muda mrefu ni kwa sababu ya rehema za Mungu na kutoiga mahusiano ya soshalaiti wengine.

"La kwanza ni neema ya Mungu kwa sababu sisi tunaomba Mungu sana, na pia tunaishi maisha yetu vile tunajua na hatutafuata maisha ya watu wengin katika jamii."

 

 

 

 

View Comments