In Summary

•Shweizer alionyesha video yake akipanda gari jeusi ambalo linaaminika kuwa Ferrari 599 GTB na kuendesha.

•Kumiliki gari la kifahari la Ferrari 599 GTB ni kidokezo tu cha jinsi mume wa Akothee  Bw Denis Shweizer alivyo tajiri.

Image: INSTAGRAM// MR OMOSH

Mume mzungu wa mwimbaji Akothee, Denis Shweizer almaarufu Mister Omosh amewaacha wanamitandao Wakenya wakiwa vinywa wazi na wakimezea mate baada ya kuchapisha video inayomuonyesha akiendesha gari zuri la kifahari.

Katika chapisho la Jumatatu, mzungu huyo alionyesha video yake akipanda gari jeusi ambalo linaaminika kuwa Ferrari 599 GTB na kuendesha..

Shweizer alitumia fursa hiyo kuwatia moyo watu kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza mambo yote wanayotaka kufikia maishani.

“Wacha tuanze wiki yenye mafanikio! Fikiri vyema, kuwa mwaminifu na rafiki kwa kila mtu. Iwe ni muuza duka katika duka kuu, mhudumu katika kituo cha mafuta, wafanyakazi wako, mshirika wako wa biashara. Fanyia kila mtu kwa uaminifu. Fanya kila mtu ajisikie muhimu. Kwa sababu kila mtu ni muhimu! Unaweza kufikia chochote! Ishi maisha yako kwa fahari,” Shweizer aliandika chini ya video hiyo aliyoiweka kwenye Instagram.

Mumewe Akothee alidokeza kuwa video hiyo ilichukuliwa wakati alipokuwa akiondoka nyumbani kuelekea kazini Jumatatu asubuhi.

Katika video hiyo, Shweizer ambaye inaaminika kuwa yupo nchini kwao, Uswizi alionekana akitoka ndani ya nyumba na kuelekea kwa gari hilo la kifahari lililokuwa limeegeshwa nje. Wakati huo, alikuwa amevaa suti ya bluu na shati nyeupe.

Mara baada ya kuingia ndani ya gari hilo, mzungu huyo aliwasha injini na kuondoka kabla ya video kuisha.

Ferrari 599 GTB ni mojawapo ya mifano adimu zaidi ya Ferrari iliyowahi kuzalishwa. Inajulikana kwa utendaji wake mzuri na injini yenye nguvu. Bei ya wastani ya Ferrari 599 GTB ni takriban dola 150, 000 hadi 200,000 (Ksh 21.5milioni- Ksh 28.8 milioni.

Kumiliki gari la kifahari la Ferrari 599 GTB ni kidokezo tu cha jinsi mume wa Akothee  Bw Denis Shweizer alivyo tajiri.

Tazama baadhi ya maoni ya wanamitandao Wakenya kwenye video ya Bw Shweizer:-

Stivebrian: Mr akotheee is driving Ferrari wueh the husband is rich.

Arnoredensen: Haha Denis what a way to start the week. 👍🏿💪🏿

Euniceshilew: the machine for me!

Gakii4800: Kwani Niko dunia pande gani?🤣🤣

Nyanchocab: Like a CEO, for sure.

View Comments